Loading...

Mnangagwa afanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri siku 2 baada ya kulitangaza

Mnangagwa afanya mabadiliko ya haraka kwenye baraza lake la mawaziri
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amefanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri siku mbili baada ya kulitangaza baraza hilo.

Wakosoaji wanasema kuwa orodha ya kwanza ilionyesha kuwa mnangagwa hakuwa na mpango wa kuleta mabadiliko nchini humo.

Wizara za elimu na kazi sasa zimefanyiwa mabadiliko ili kuambatana na katiba.

Lakini makamanda wa jeshi ndo walipewa wizara za mashauri ya nchi za kigeni na ardhi.

Siku 10 zilizopita alirudi kutoka uhamishoni kufuatia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Robert Mugabe na kuahidi kuhudumia raia wote kwa njia sawa.

Siku ya Jumamosoi serikali ilitangaza kuwa wizara mbili zemefanyiwa mabadiliko kuhakikisha kuwa katiba imefuatwa kwa misingi na jinsia, kikanda na mahitaji maalumu.

Ripoti zinasema kuwa orodha kwanza hakufuata katiba ambayo inataka kuwepo mawaziri wasiokuwa wabunge.

Baadhi ya wafuasi wa upinzani walisherehekea hatua ya kumuona waziri wa elimu Lazarus Dokora akiondolewa wakisema amechangia kushuka kwa viwango vya elimu miaka michache iliyopita.

Naibu wake Paul Mavima amechukua mahala pake.
Mnangagwa afanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri siku 2 baada ya kulitangaza Mnangagwa afanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri siku 2 baada ya kulitangaza Reviewed by Zero Degree on 12/03/2017 02:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.