Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 3 Decemba, 2017

Kiungo wa Timu ya Taifa na Uingereza na klabu ya Everton, Ross Barkley
Sam Allardyce anataka kumbakisha Ross Barkley lakini anadai kuna uwezekano mkubwa kwamba dili la uhamisho wa Kiungo huyo wa Uingereza kuondoka katika klabu ya Everton tayari lilishakamilika.

Ronald Koeman amesema kwamba alikataaa ofa kadhaa kutoka baadhi ya vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutimuliwa Everton. (Skysports)

Manchester United wako tayari kuachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale isipokuwa Real Madrid ikipunguza bei ya mchezaji huyo.

Tottenham wametangaza kwamba, paundi milioni 50 ndio bei ya kwanza kwa klabu itakayotaka kumsajili Danny Rose, mwezi Januari.

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amefanikiwa kukwepa adhabu ya Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kwa kuwatakia majeruhi wapinzani wake, Manchester City.

Leon Goretzka
Mchezaji anayewindwa na Liverpool, Arsenal na Manchester City, Leon Goretzka amepewa ofa itakayovunja rekodi katika klabu ya Schalke 04 itakayomfanya alipwe zaidi ya paundi 150,000 kwa wiki.

Meneja mpya wa Everton, Sam Allardyce anatazamia kuwasajili Steven N'Zonzi na Troy Deeney mwezi Januari.

Manchester City wako tayari kukataa ofa zote za mkopo kwa chipukizi wao, Phil Foden mwezi Januari.

Rangers wanatarajiwa kuchanganywa na jaribio lao la kutaka kumsajili Scott McTominay kwa mkopo baada ya Jose Mourinho kusema kwamba, kiungo huyo ana majukumu Old Trafford. (Mirror)

Joe Hart
David Moyes amekiri kwamba, nafasi ya Joe Hart kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza iko matatani kufuatia hali mbaya inayoiandama klabu ya West Ham.

Meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardyce ameupa kipaumbele mpango wa kusajili mshambuliaji mwezi Januari.

Mji wa Stockholm unatarajiwa kuupiku mji wa Brussels kwenye orodha ya miji inayotarajiwa kuwa wenyeji wa michuano ya Euro 2020. (Daily Mail)

Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) linaficha jedwari lao la 'fair-play' kuzilinda klabu zilizofanya vibaya - klabu ya Burnley ikitangaza kwamba wiki iliyopita ilifanikiwa kushinda paundi 20,000 kwa kuwa na rekodi nzuri. (Observer)

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ana matumaini ya kumfanya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang akubali kusaini mkataba na klabu yake mwezi Januari.

Jonny Evans
Manchester City hawajakata tamaa ya kumsajili beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans. (Express)

Raheem Sterling anatarajia kuanza kulipwa paundi 300,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester City, wakati klabu hiyo ikifikiria kumpa Fabian Delph ofa ya mkataba mpya.

Chelsea wako tayari kumwachilia Thibaut Courtois aondoke kama mchezaji huru mwaka 2019 zaidi ya kukubali kumuuza kwa klabu ya Real Madrid kwa dau nono mwakani.

Meneja wa Crystal Palace, Roy Hodgson anataka kumsajili golikipa wa klabu ya Paris Saint-Germain, Kevin Trapp.

klabu ya Shanghai Shenhua ya China inatarajiwa kumpa ofa Aleksandar Mitrovic itakayomshawishi aachane na klabu yake ya Newcastle.

Nyota wa klabu ya Chelsea ya wanawake, Eniola Aluko alikimbizwa hospitali baada ya kujigonga kwenye bango la matangazo katika mechi yao dhidi ya Yeovil.

Matumaini ya Manchester United kumsajili Gareth Bale yamekufa baada ya Real Madrid kudai inamhitaji nyota huyo aje kuwa mkombozi kutokana na hali mbaya waliyonayo msimu huu.

Lukas Nmecha
Klabu ya Everton ina matamanio makubwa ya kumsajili chipukizi wa Manchester City, Lukas Nmecha.

Mshambuliaji wa Derby, Chris Martin ni kinara kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na klabu ya Wolves Januari.

Klabu ya Manchester United imeonyesha kutofurahishwa na kitendo cha beki wake, Timothy Fosu-Mensah ambaye yuko Crystal Palace kwa mkopo kupewa muda kidogo uwanjani. (Sun)

Henrikh Mkhitaryan atakaribishwa kwa mikono miwili Borussia Dortmund kama atashindwa kuifanya Manchester United impe nafasi ya kudumu.

Manchester City wana wasiwasi wa kuchukua tahadhari za kinidhamu kwa nyota wao Vincent Kompany, Leroy Sane na Fernandinho kuelekea mechi yao dhidi ya West Ham - ambao wote watatu wamebakiza kadi moja tu ya njano ambayo itawafanya wafungiwe na kuikosa 'derby' ya wikendi ijayo. (Star)

Toby Alderweireld
Toby Alderweireld anasema kwamba tarehe ya kurejea kwake kutoka majeruhi haijulikani kwa sababu yuko katika hatari ya kuchelewa kurejea kikosini.

Rangers wataongeza dau kwenye ofa yao ya awali kumfanya meneja Derek McInnes aachane na klabu ya Aberdeen wiki hii. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 3 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 3 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/03/2017 02:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.