Loading...

Orodha ya mabeki 10 ghali zaidi Duniani, namba moja ni Virgil van Dijk


Kitendo cha klabu ya Liverpool kufanikisha dili la uhamisho wa Virgil van Dijk kimevunja rekodi ya ada ya uhamisho wa beki katika historia ya soka.

Muholanzi huyo anaondoka Southampton kwenda Anfield kwa dau la pauni milioni 75.

Dili hilo litakamilika rasmi tarehe 1 Januari, 2018, wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa, ambapo rekodi ya klabu ya Manchester City ya kufanya usajili wa beki kwa dau kubwa ikitarajiwa kuvunjwa.

Vinara hao wa EPL walishikilia rekodi hiyo baada ya kumsajili Kyle Walker kutoka Tottenham kwa dau la pauni milioni 54.

Na pia, Pep Guardiola kumsajili beki wa klabu ya Monaco, Benjamin Mendy kwa dau la pauni milioni 52 kwenye majira ya joto.

Liverpool inathibitisha kumnasa Virgil van Dijk baada ya klabu ya Southampton kuikubali ofa yao ya pauni milioni 75.


Liverpool wanaonekana kumthamini kupita kipimo beki huyo mwenye umri wa miaka 26, wakati Manchester City wakionekana kuwa kuwa na kila sababu ya kuitwa mabingwa wa 2017/18, huku Jurgen Klopp na vijana wake wakiwa wamebakiza Kombe moja tu la kushindania.

Hivi ndivyo Van Dijk naye anavyoingia kwenye orodha ya mabeki 10 ghali zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya soka duniani, huku karibu nusu yao ikiwa ni ya wachezaji wa Manchester City.

10. Eliaquim Mangala, kutoka Porto kwenda Manchester City, pauni milioni 32


9. Thiago Silva, kutoka AC Milan kwenda PSG, pauni milioni 33


8. David Luiz, kutoka PSG kwenda Chelsea, pauni milioni 34


7. Shkodran Mustafi, kutoka Valencia kwenda Arsenal, pauni milioni 35


6.
Leonardo Bonucci, kutoka AC Milan kwenda Juventus, pauni milioni 35.2


5. John Stones, kutoka Everton kwenda Manchester City, pauni milioni 47.5


4. David Luiz, kutoka Chelsea kwenda PSG, pauni milioni 50


3. Benjamin Mendy, kutoka Monaco kwenda Manchester City, pauni milioni 52


2. Kyle Walker, kutoka Tottenham kwenda Manchester City, pauni milioni 54


1.
Virgil van Dijk, kutoka Southampton kwenda Liverpool, pauni milioni 75

Van Dijk amefanikisha uhamisho aliokuwa akiulilia kwa muda mrefu
Orodha ya mabeki 10 ghali zaidi Duniani, namba moja ni Virgil van Dijk Orodha ya mabeki 10 ghali zaidi Duniani, namba moja ni Virgil van Dijk Reviewed by Zero Degree on 12/28/2017 05:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.