Loading...

Yanga yamkingia kifua Obrey Chirwa


Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, umesema mshambuliaji wake, Obrey Chirwa atareja nchini siku yoyote baada ya kwisha kwa msiba wa mtoto wa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina.

Chirwa aliondoka nchini baada ya kuomba ruhusa kurejea kwao Zambia kwa masuala ya kifamilia. Lakini baadaye akagoma kurejea nchini akitaka kumaliziwa fedha zake za usajili.

Hali hiyo ilisababisha hali ya sintofahamu na Chirwa akaendelea kubaki Zambia huku akionekana mitandaoni akiendelea na kilimo cha mahindi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum Nyika amesema kilichomkwamisha Chirwa ni msiba wa mtoto wa kocha.

"Alikuwa bado Zambia, baada ya kusikia kocha ana msimba, alilazimika kubaki kule kumliwaza," alisema akionekana kutaka kupoza kidogo joto la Chirwa kubaki Zambia kwa mgomo.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba, uongozi wa Yanga umemalizana naye kwa kumpatia kiasi cha fedha zake za usajili na umekubaliana naye kurejea haraka.
Yanga yamkingia kifua Obrey Chirwa Yanga yamkingia kifua Obrey Chirwa Reviewed by Zero Degree on 12/28/2017 04:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.