Loading...

TFF yakanusha taarifa hii


Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha taarfia zinazosambaa zikipotosha kauli ya Rais Wallace Karia kuhusu kuzuia mashindano ya soka yasiyo rasmi.

Taarifa ya TFF imeeleza kuwa watu wanamnukuu vibaya Rais Karia kwani hakusema shirikisho hilo linafuta mashindano bali zinaandaliwa kanuni ambazo zitatakiwa kufuatwa na waandaaji wa mashindano hayo.

“TFF inaandaa kanuni ili mashindano yote ya aina hiyo yakidhi vigezo katika utaratibu mzuri na watapata vibali kupitia FA Wilaya na Mikoa baada ya kutimiza vigezo vitakavyowekwa”, imeeleza sehemu ya taarifa ya TFF.

Mapema jana Karia mbele ya wahariri wa habari za michezo, alieleza dhamira hiyo ya TFF katika kuweka utaratibu utakaoboresha mashindano hayo.

TFF yakanusha taarifa hii TFF yakanusha taarifa hii Reviewed by Zero Degree on 12/28/2017 04:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.