Loading...

Rio Ferdinand ataja mchezaji wa EPL ambaye alichukia kucheza naye kama mpinzani

Rio Ferdinand alichukia kucheza dhidi ya Eden Hazard
Rio Ferdinand amemtaja Eden Hazard kama mchezaji wa Ligi Kuu ya Uingereza ambaye alichukia kucheza naye kama mpinzani na bado huwa anamtokea kama jinamizi akilala.

Mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye amekuwa katika kiwango cha juu zaidi kwa misimu kadhaa iliyopita, anaitia wazimu sana klabu ya Real Madrid ambayo itakuwa makini sana katika kujaribu kamsajili nyota huyo kwenye majira ya joto.

Alicheza dhidi ya Ferdinand akiwa anamalizia maisha yake ya soka katika klabu ya Manchester United, ambaye uwezo wake haukuwa kama alivyokuwa awali.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji na klabu ya Chelsea, Eden Hazard
Na uwezo wa Mbelgiji huyo kisoka, ukiongeza kasi aliyonayo na nguvu zake katika miguu vilmteza sana Mwingereza huyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'BT Sport', Ferdinand alisema: "Sikuwahi kufurahia kucheza dhidi ya Hazard, bado namkumbuka sana na huwa ananitokea kama jinamizi."

"Nilifurahia tu kwamba alicheza kwa mapana… akiwa chini ya Jose Mourinho alikuwa upande wa kushoto kwa sana hivyo hakuja upande wangu mimi na ilikuwa ahueni kwangu.

"Lakini kwa sasa tunamshuhudia katika safu nzima ya ushambuliaji, kwa kweli anakuvutia kumtazama na ndiye anayeipa nguvu klabu ya Chelsea."

Hazard alikuwemo kwenye kikosi cha Chelsea kilichocheza dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa wa hatua ya makundi, mchezo uliomalizika kwa sare ya goli 1-1.
Rio Ferdinand ataja mchezaji wa EPL ambaye alichukia kucheza naye kama mpinzani Rio Ferdinand ataja mchezaji wa EPL ambaye alichukia kucheza naye kama mpinzani Reviewed by Zero Degree on 12/06/2017 02:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.