Loading...

Marekani yaionyesha ubabe Korea Kaskazini

Ndege ya Jeshi la Marekani ya B-1B bomber, yaionyesha ubabe Korea Kaskazini
Jeshi la Marekani limerusha ndege yake aina ya B-1B bomber katika anga la Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini.

Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani.

Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu kuonyesha ubabe baada ya majaribio ya makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini.

Zaidi ya ndege 200 na maelfu ya wanajeshi wanashiriki katika mazoezi hayo ya kijeshi ambayo yatakamilika siku ya Ijumaa.

Pyongynag ambayo mara nyingi hukashifu mazoezi ya pamoja ya Marekania na Korea Kusini, imeyataja mazoezi ya sasa kuwa ni uchokozi wa vita vya nyuklia.

Misukosuko imekuwa ikiongezeka tangu lifanyike jaribio la kombora mwezi uliopita lililosababisha lawama za kimataifa na onyo kutoka Marekani kuwa Korea Kaskazini itaharibiwa kabisa ikiwa vita vitatokea.
Marekani yaionyesha ubabe Korea Kaskazini Marekani yaionyesha ubabe Korea Kaskazini Reviewed by Zero Degree on 12/06/2017 02:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.