Loading...

Alichokifanya Eden Hazard baada ya klabu ya Real Madrid kujitokeza kutaka kumsajili

Mshambuliaji wa Klabu ya Chelsea, Eden Hazard
Eden Hazard ameripotiwa kukataa kusaini mkataba mpya na klabu ya Chelsea.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza wana matamanio makubwa ya kumfanya Hazard akubali kusaini mkataba mpya licha ya kwamba mkataba wake wa sasa unamfanya nyota huyo aendelee kubakia Stamford bridge kwa muda wa miaka miwili na nusu ijayo.

Hazard amekuwa kivutio kwa klabu ya Real Madrid huku Zinedine Zidane akiwa na matamnio makubwa ya kumsajili Mbelgiji huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na 'Times', Chelsea walikuwa tayari kumpa Eden Hazard mshahara wa paundi 300,000 kwa wiki, ambapo angevunja rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kulipwa fedha nyingi na klabu ya Chelsea katika historia ya soka.

Lakini taarifa zinadai kwamba, Hazard amekataa ofa hiyo akiwa na matumaini ya kufanikiwa kuhamia Bernabeu.

Mbelgiji huyo alionyesha uwezo wake katika mechi ya Chelsea Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne usiku ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Chelsea walifanikiwa kuondoka na pointi moja tu, ambayo iliwapa nafasi ya kusonga katika hatua inayofuata ya mtoano ingawa walimaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi C.

Rio Ferdinand aliulizwa kuhusu kiwango cha Hazard kwa sasa, na kukiri kwamba alipata wakati mgumu sana kumkabili Mbelgiji huyo katika enzi zake.

"Sikuwahi kufurahia kucheza dhidi ya Hazard, bado namkumbuka sana na huwa ananitokea kama jinamizi," Ferdinand aliiambia 'BT Sport'

"Nilifurahia tu kwamba alicheza kwa mapana… akiwa chini ya Jose Mourinho alikuwa upande wa kushoto kwa sana hivyo hakuja upande wangu mimi na ilikuwa ahueni kwangu.

"Lakini kwa sasa tunamshuhudia katika safu nzima ya ushambuliaji, kwa kweli anakuvutia kumtazama na ndiye anayeipa nguvu klabu ya Chelsea."
Alichokifanya Eden Hazard baada ya klabu ya Real Madrid kujitokeza kutaka kumsajili Alichokifanya Eden Hazard baada ya klabu ya Real Madrid kujitokeza kutaka kumsajili Reviewed by Zero Degree on 12/06/2017 08:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.