Loading...

Star Media yapigwa faini ya shilingi milioni 100 kwa kutoza fedha chaneli za bure


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeitoza faini ya Sh100 milioni kampuni ya Star Media kwa kuwatoza fedha watazamaji wa chaneli zinazotakiwa kuonekana bila kulipiwa kupitia king’amuzi cha Star Times.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema kitendo hicho ni kinyume cha kanuni ya 14(2) (a) ya kanuni za Digital and Broadicasting Networks za mwaka 2011.

“TCRA inaendelea kufuatilia kuhakikisha kuwa ving’amuzi vya Star Times, Continental, Digitek na Ting vinaendelea kuonyesha chaneli zote za kitaifa za FTA (Free to Air) bure kwa mujibu wa sheria,” alisema Kilaba. 

Chaneli zinazotakiwa kuonekana bila kulipiwa ni TBC1, ITV, EATV, Channel Ten, Star TV na Clouds TV. Kampuni hiyo imetozwa faini kuanzia Desemba 22 na inatakiwa kuwa imelipa kabla ya Januari 30.

Akizungumzia uamuzi huo, mkazi wa jijini Mwanza, Pius Rugonzibwa alipongeza akisema wamekuwa wakipata usumbufu kwa kukatiwa huduma.
Star Media yapigwa faini ya shilingi milioni 100 kwa kutoza fedha chaneli za bure  Star Media yapigwa faini ya shilingi milioni 100 kwa kutoza fedha chaneli za bure Reviewed by Zero Degree on 12/30/2017 12:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.