Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 1 Decemba, 2017
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Kevin De Bruyne |
Klabu ya Real Madrid imefanya mawasiliano na wakala wa Kevin De Bruyne kuhusiana na uwezekano wa uhamisho wa nyota huyo wa Manchester City.
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amewaambia skauti wake wamtafutie "mchawi" katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Tottenham wako tayari kujaribu kumsajili kiungo wa klabu ya West Ham, Manuel Lanzini.
Emerson Palmieri anayewindwa na Liverpool amesema hana mpango wa kutua Anfield, akisistiza kwamba anafurahia kuwa na klabu ya Roma.
Mshambuliaji wa Liverpool, Divock Origi amaesema anaweza kuondoka Liverpool kwa kusaini mkataba wa kudumu Ujerummani. (Sun)
Arda Turan |
Barcelona wako tayari kumtumia kiungo wa Timu ya Taifa ya Uturuki, Arda Turan kuishawishi Arsenal kumuuza Mesut Ozil.
Lionel Messi amesababisha mgawanyiko katika klabu ya Barcelona baada ya kuuomba uongozi wa klabu huyo umsajili nyota wa klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho.
Bryan Cristante |
Manchester United wanatarajia kumsajili kiungo wa klabu ya Atalanta kwa paundi milioni 31, Bryan Cristante kama mbadala wa Marouane Fellaini.
Gareth Southgate amemsakama meneja wa Manchester United, Jose Mourinho kwa kile anachodai kwamba hamtendei haki Phil Jones. (Star)
Klabu za Arsenal na Manchester City zinatarajiwa kushindania saini ya Nahodha wa West Brom, Jonny Evans mwezi Januari.
Danny Welbeck |
Arsene Wenger anafikiria kumchagua Danny Welbeck badala ya Olivier Giroud kwenye mchezo wao dhidi ya Manchester United siku ya Jumamosi licha ya mfaransa huyo kufunga goli mbili katikati ya wiki na kukosekana kwa Alexandre Lacazette. (Telegraph)
Arsenal wako tayari kutoa ofa kwa ajili ya kumnasa Jonny Evans ikiwa ni katika harakati za kuimarisha safu yao ya ulinzi mwezi Januari.
Gareth Southgate amewatetea madaktari wa Timu ya Taifa ya Uingereza juu ya matibabu ya Phil Jones.
Ofa Liverpool kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya Roma, Emerson Palmieri imekutana pigo baada ya beki huyo kukiri kwamba anafurahia kuwa klabu yake hiyo ya nchini Italia. (Mirror)
Mashabiki wa soka wa Uingereza watakumbana na adhabu ya kufungwa miaka 15 jela nchini Urusi kama watashiriki katika vitendo vya uvunjifu wa amani katika Kombe la Dunia mwakani.
Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Uingereza |
Klabu ya Tottenham imemwajiri raia wa Uingereza, Chris Powell katika timu yao ya maskauti.
Emre Can amesistiza kwamba mgogoro wake juu ya mkataba mpya hauhusiani na fedha na kusdai kwamba anaweza kusaini mkataba mpya nakatika klabu ya Liverpool au na klabu nyingine mwezi Januari. (Daily Mail)
Gareth Southgate amaemtaka Harry Kane athibitishe kwamba yeye ni straika wa kimataifa kwa kufanya maajabu kwenye kombe la dunia mwakani.
Gareth Southgate amaemtaka Harry Kane athibitishe kwamba yeye ni straika wa kimataifa kwa kufanya maajabu kwenye kombe la dunia mwakani.
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Celtic, Charlie Nicholas anaamini Scott Sinclair alikuwa na bahati kwa kukwepa adhabu ya kujiangusha. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 1 Decemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
12/01/2017 06:49:00 PM
Rating: