Loading...

Rais mpya wa Zimbabwe atangaza baraza lake la mawaziri

Rais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri
Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ametangaza baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake.

Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo, Jenerali aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.

Mkuu wa jeshi la angani, Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha na kilimo.

Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.

Bwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliyopita kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka saba.

Upinzani umelaumu mabadiliko hayo kama usaliti wa matumaini miongoni mwa raia na thibitisho kuwa vikosi vya usalama vilivyokuwa na nguvu nyingi wakati wa utawala wa Mugabe vinaendelea kuthibiti taifa hilo.

Hali ya kuleta uwiano na umoja iliyoonekana katika siku za karibuni huenda ikabadilishwa na makabiliano ya uongozi katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Rais mpya wa Zimbabwe atangaza baraza lake la mawaziri Rais mpya wa Zimbabwe atangaza baraza lake la mawaziri Reviewed by Zero Degree on 12/01/2017 12:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.