Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 2 Decemba, 2017
Raheem Sterling na Pep Guardiola |
Pep Guardiola amekiri kwamba, Manchester City ilifanya jambo sahihi kuacha kumuuza Raheem Sterling kwenda Arsenal katika kipindi cha majira ya joto kilichopita.
Jurgen Klopp anasistiza kwamba Philippe Coutinho anabakia kuwa mchezaji muhimu wa klabu ya Liverpool baada ya kufanikiwa kuzima mipango ya awali ya klabu ya Barcelona kujaribu kumshawishi Mbrazil huyo.
Arsene Wenger amezungumzia umakini wa safu ya ulinzi wa klabu ya Arsenal lakini yuko tayari kwa hilo kufanyiwa majaribio katika mechi yao dhidi ya klabu ya Manchester United. (Mirror)
Mauricio Pochettino akizungumza na Toby Alderweireld |
klabu ya Tottenham haitaki kubwetekea mfumo wake mzuri wa ulipaji mishahara ikihofia kumpoteza beki wake, Toby Alderweireld.
Liverpool imekumbana na pigo kubwa kufuatia kiungo wa klabu hiyo, Joel Matip kupata majeraha yatakayomweka nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.
Aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Ruud Gullit anasistiza kwamba, Uingereza lazima wafanye vizuri na kusema kuwa chaguo lake la kwanza kwenye Kombe la Dunia ni Timu ya Taifa ya Ufaransa. (Daily Mail)
Meneja mpya wa Klabu ya everton, Sam Allardyce |
Sam Allardyce anasema kwamba, matamanio yake makubwa ni kuwa na klabu ya Everton kwa zaidi ya miezi 18 ya mkataba wake wa sasa. (Guardian)
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anataka kumsajili Mesut Ozil katika majira ya joto yajayo akitazamia kumaliza tatizo la nafasi ya namba 10 Old Trafford. (Telegraph)
Mesut Ozil amezidisha uvumi wa kwamba anweza kurejea katika klabu ya Real Madrid baada ya kufichua kwamba anafanya mawasiliano na Zinedine Zidane.
Emre Can amekiri kwamba, mwisho wa siku anaweza kukubali kusaini makataba mpya na klabu ya Liverpool licha ya kwamba klabu ya Juventus imeonyesha matamanio makubwa ya kumsajili.
Nyota anayewindwa na klabu ya Chelsea, Alex Sandro amesema kwamba ana mpango wa kuondoka Juventus katika kipindi cha majira ya joto kichajo.
Ahmed Hegazi |
West Brom wanahofia kunpoteza beki waliyemsajili kwa mkopo, Ahmed Hegazi ingawa mkataba wao una kipengele kinachowawezesha kumnunua nyota huyo mwishoni mwa msimu huu. (Sun)
Meneja mpya wa klabu ya Everton, Sam Allardyce ametupilia mbali rekodi za Marco Silva na kusistiza kwamba yeye ni bora zaidi katika nafasi hiyo.
Derek McInnes amekanusha kwamba uvumi wa yeye kutimkia Rangers umespelekea matokeo mabovu katika klabu ya Aberdeen. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 2 Decemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
12/02/2017 10:52:00 AM
Rating: