Loading...

Makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2018


Nigeria wamepangwa kwenye kundi moja na Argentina kwa mara nyingine, Misri nao wamepangwa na wenyeji Urusi na Uruguay baada ya droo ya Kombe la Dunia 2018 kufanywa nchini Urusi.

Panama, ambao wanacheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza wamepangwa kwenye kundi moja na Ubelgiji, Uingereza na Tunisia.

Taifa la Iceland, lililoshangaza watu wengi kwa kufuzu, limepangwa 
katika Kundi D pamoja na Nigeria, Croatia na Argentina.

Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Urusi na Saudi Arabia.


Droo kamili ya Kombe la Dunia:
  • Kundi A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay
  • Kundi B: Ureno, Uhispania, Morocco, Iran
  • Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark
  • Kundi D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria
  • Kundi E: Brazil, Uswizi, Costa Rica, Serbia
  • Kundi F: Ujerumani , Mexico, Sweden, Korea Kusini
  • Kundi G: Ubelgiji , Panama, Tunisia, England
  • Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan.
Makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Reviewed by Zero Degree on 12/02/2017 09:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.