Loading...

Wema Sepetu atimka rasmi Chadema, ..CCM yamtolea nje


Muigizaji wa filamu za kibongo na Miss Tanzania 206 Wema Sepetu ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi huku akidai kwamba hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amesema kwamba anatangaza rasmi kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho alitangaza kujiunga nacho Februari mwaka huu

Ujumbe aliandika Wema Kwenye ukurasa wake wa Instagram
"Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani" . Wema Sepetu.

Baada ya Muigizaji huyo kutangaza kurudi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho hakina taarifa yoyote ya kurudi kwa Wema Sepetu.

Polepole amesema CCM ina utaratibu wa mwanachama kujiunga na chama hicho na kuongeza kwamba chama chao siyo daladala kwamba mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote apendao, na kwamba CCM ina misingi, imani na masharti ya uanachama.

"Kupitia utaratibu na muundo wetu wa chama kwenye shina kisha ataandikwa kwenye orodha ya wanachama kwenye tawi ambalo yeye ni mkaazi," amesema Polepole.

Ameongeza kwamba habari za Muigizaji huyo kurudi ndani ya CCM yeye amepata taarifa mitandaoni kama jinsi watu wengine walivyozipata.

Pamoja na hayo polepole amefafanua kuwa "Ni heri abaki huko huko (Chadema) au akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu, Kuijenga CCM mpya yenye kuheshimu nidhamu ya chama siyo kazi ndogo na inataka viongozi wenye unyenyekevu, watumishi na wanachama wavumilivu. CCM mpya itakuwa chungu kwa baadhi yetu lakini tamu kwa wengi wetu"
Wema Sepetu atimka rasmi Chadema, ..CCM yamtolea nje Wema Sepetu atimka rasmi Chadema, ..CCM yamtolea nje Reviewed by Zero Degree on 12/02/2017 09:43:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.