Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 24 Decemba, 2017

Mkufunzi wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger bado ana nia ya kumsajili Steven N'Zonzi dirisha dogo litakapofunguliwa.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amemfanya beki wa kati wa klabu ya Inter Milan, Milan Skriniar kuwa chagu lake la kwanza kwenye usajili wa mwezi Januari.

Mauricio Pochettino yuko tayari kusajili wachezaji wawili mwezi Januari, akiwemo Ross Barkley na Luke Shaw kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Tottenham.

Liverpool wanakaribia kukubaliana na Southampton juu ya usajili wa Virgil van Dijk kwa paundi milioni 70. (Express)

Manchester United wanakawiza mkataba mpya wa meneja wao Jose Mourinho.

Dele Alli 
Kwa mujibu wa Jermaine Jenas, Dele Alli ataondoka Tottenham kama Real Madrid au Barcelona watajaribu kumsajili kwenye majira ya joto.

Arsenal wako mstari wa nbele kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota wa Bayer Leverkusen, Leon Bailey ambaye ana kadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 30 - na wako tayari kumsajili mwezi ujao.

Wakala wa Olivier Giroud yuko London kwa ajili ya mazungumzo juu ya future ya mshambuliaji huyo wa klabu ya Arsenal.

Liverpool, Tottenham na Everton zote zinatazamia kumsajili kiungo wa Sheffield United, David Brooks ambaye ana thamani ya paundi milioni 20.

Meneja wa klabu ya Sunderland, Chris Coleman ana matumaini ya kuungana na nyota wa Timu ya Taifa ya Wales na klabu ya Liverpool, Ben Woodburn kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Alexis Sanchez alionekana kuvutiwa na mkataba mpya Arsenal, lakini alibadili uamuzi wake baada ya kupoteza mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich (Mirror)

Joe Hart ana nia ya kurejea Italy mwezi January kulinda nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza cha Kombe la Dunia.

Jose Mourinho yuko tayari kuhakikisha anakamilisha usajili wa Ryan Sessegnon kutoka Fulham kuja Manchester United kwa paundi milioni 25.

Rafa Benitez atasikiliza ofa zitakazotolewa kwa ajili ya Jack Colback, Mohamed Diame na Rolando Aarons mwezi Januari.

Steven N'Zonzi
Meneja wa West Ham, David Moyes anakumbana na ushindani mkubwa ambao utamfanya ashindwe kufanikisha usajili wa Steven N'Zonzi - lakini ana tazamia kushtukiza usajili wa kiungo wa Scotland, John McGinn.

Chelsea wanataka kumrejesha Mason Mount kutoka Vitesse Arnhem ambako yuko kwa mkopo. (Sun)

Pep Guardiola ana nia ya kumsajili nyota wa Shakhtar Donetsk, Fred akiwa kwenye mikakati ya kuboresha safu ya kiungo Manchester City kwenye majira ya joto.

FIFA imeahidi kuchunguza tuhuma zinazoikabili Urusi kabla ya Kombe la Dunia mwaka 2018 - kitendo kinachoweza kuiangamiza Timu ya taifa ya Urusi ambayo iko chini ya kiwango hadi hivi sasa. (Daily Mail)

Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amefunga milango kwa ya Kombe la Dunia kwa Jack Wilshere.

Nyota wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah anataka kuhamia Real Madrid na tayari amemwambia wakala wake ashughulikie dili hilo.

Daniele Rugani
Arsenal na Manchester Utd kushindania saini ya nyota wa klabu ya Juventus, Daniele Rugani, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 35.5.

Tottenham inataka kumsajili beki wa Manchester United, Luke Shaw na kiungo wa Everton, Ross Barkley mwezi Januari.

Nyota wa klabu ya Ajax, Frenkie de Jong ni kiungo pekee aliyefuatiliwa na Man City hivi karibuni. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 24 Decemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 24 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/24/2017 04:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.