Loading...

Utabiri wa Eden Hazard, Chelsea Vs Barcelona

Hazard atabiri ushindi kwa Chelsea
Eden Hazard ametabiri matokeo ya mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa kati ya Chelsea dhidi na Barcelona.

Eden Hazard ana matumaini Chelsea itaitoa Barcelona nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani.

Hazard ana matumaini ya kuisaidia Chelsea kupata taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa tangu ajiunge na klabu hiyo kwenye majira ya joto mwaka 2012.

Lakini Mbelgiji huyo amekiri kwamba 'The Blues' wanakutana na jaribio kubwa dhidi ya vigogo hao wa La Liga.

Akizungumza kwenye mahojiano na Sky Sports, Hazard alisema: “Kila mwaka najaribu kuwa bora zaidi. Nataka kuwa bora zaidi, na kucheza na timu bora zaidi, hivyo wakati mwaka mpya unaingia, azimio langu ni kuwa bora zaidi na kushinda mataji. Hiyo ni sehemu ya kazi yangu.

“Tunacheza vizuri kwa sasa. Nataka kuendelea mbele na kushinda mataji zaidi. Kushinda Kombe la Dunia na Ubelgiji ni jambo kubwa, lakini pia Taji la Ligi ya Mabingwa na Chelsea.

“Nachotaka ni kupenya, najua sio rahisi kwa sababu sasa tuko na Barcelona.

“Hivyo, tutaona itakavyokuwa. Nataka kufurahia mchezo kama nilivyofanya mwaka huu, na kujaribu kuwafurahisha mashabiki.”
Utabiri wa Eden Hazard, Chelsea Vs Barcelona Utabiri wa Eden Hazard, Chelsea Vs Barcelona Reviewed by Zero Degree on 12/24/2017 02:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.