Loading...

Yanga SC yaanza kufuata nyayo za Simba

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga
Klabu ya Yanga ambao ndio mabigwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, imeteua kamati ya mabadiliko yenye watu sita akiwemo mkuu wa mkoa wa zamani wa Dar es salaam Mh. Meck Sadick.


Yanga SC imefikia hatua hiyo kwa kufuata za mahasimu wao, Klabu ya Simba kwa kuunda kamati hiyo ya mabadiliko ambayo itasimamia mchakato wa kuelekea kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu kuwa wa Hisa.

Akitaja kamati hiyo leo Desemba 22, 2017, Kaimu Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Clement Sanga amesema kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni mwanasheria, Alex Mgongolwa.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Prof. Mgongo Fimbo ambaye ni mtaalam wa Katiba na sheria za ardhi, RC wa zamani wa Dar es salaam, Meck Sadick na Mohamed Nyenge ambaye ni mchumi na Mwenyekiti wa kamati ya uchumi na fedha wa Yanga.

Kamati ya mabadiliko – Yanga SC iliotangazwa leo hii na Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga kwenye mkutano na waandishi wa habari.
  1. Alex Mgongolwa – m/kiti – mwanasheria
  2. Prof Mgongo Fimbo – mtaalam wa katiba na sheria za ardhi
  3. Meki Sadiki – mkuu wa mkoa mstaafu
  4. Mohamed Nyenge – mchumi na m/kiti kamati ya uchumi na fedha – Yanga
  5. George Fumbuka – mshauri masuala ya uwekezaji
  6. Felix Mlaki – mchumi na mtaalam wa masuala ya fedha
Yanga SC yaanza kufuata nyayo za Simba Yanga SC yaanza kufuata nyayo za Simba Reviewed by Zero Degree on 12/22/2017 08:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.