Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 22 Decemba, 2017

Mario Balotelli 
Mshambuliaji wa Nice, Mario Balotelli anataka kuhamia timu kubwa kama mchezaji huru na tayari ameichagua klabu ya Manchester City.

Lamine Kone anaweza kuhamia Everton kwa dau la paundi milioni 10 mwezi Januari - na wakati Sunderland ilikataa ofa ya paundi milioni 19 kutoka klabu hiyo ya Goodison Park katika kipindi cha majira ya joto kilichopita. (Mirror)

Manchester United wanamfuatilia winga wa klabu ya Borussia Dortmund, Christian Pulisic.

Manchester City ina uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez kwenye majira ya joto na inatazamia kusajili kiungo mkabaji na beki wa kati.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola ametajwa kwenye ripoti ya polisi wanaofanya uchunguzi wa sakata la uhuru wa Catalan.

Mshambuliaji wa Newcastle, Aleksandar Mitrovic anawindwa na klabu ya West Bromwich Albion.

Mkurugenzi wa michezo wa Everton, Steve Walsh na skauti mkuu wa klabu hiyo, Martyn Glover walikuwa Lille siku ya Jumatano usiku kumchunguza Bakary Soumaoro akicheza dhidi ya Nice.

Sam Allardyce anatarajiwa kumzuia mshambuliaji Sandro na kiungo James McCarthy kuondoka Everton mwezi Januari baada ya kuvutiwa na kiwango walichoonyesha kwenye mechi iliyochezwa bila mashabiki Jumanne .

Burnley wamerejea kinyang'anyiro cha kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Bordeaux, Nicolas de Preville.

Jack Wilshere
Marseille wameingia kwenye orodha ya vilabu vyenye nia ya kumsajili kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere.

Lewis Morgan ataachana na uhamisho kwenda Nottingham Forest na Preston North End akubali uhamisho wa paundi 300,000 kutoka St Mirren kwenda Celtic wiki ijayo. (Daily Mail)

Arsenal watatoa ofa ya paundi milioni 35.4 kumleta nyota wa klabu ya Juventus, Daniele Rugani kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester United wako tayari kuingia hasara kwa kumruhusu Henrikh Mkhitaryan arejee Borussia Dortmund kwa mkopo.

Ushindani wa Arsenal, Everton na West Ham kuwania saini ya kiungo Steven Nzonzi umezimwa na dau ambalo klabu ya Sevilla inalihitaji. (Sun)

Chelsea imempa ofa Thibaut Courtois ya kuwa golikipa anayelipwa pesa nzuri duniani kwa kumpa mkataba utakaomwingizia zaidi ya paundi 200,000 kwa wiki.

Swansea City ina hofia kupoteza mchezaji mwingine wa muhimu kikosini baada ya West Ham kuonyesha nia ya kutaka kuanzisha mkakati wa kumsajili beki wa kati wa klabu hiyo, Alfie Mawson. (Telegraph)

Pep Guardiola ameuambia uongozi wa Manchester City kwamba anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez na Virgil van Dijk wa Southampton, ikieleweka kuwa wote hao wako kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na viongozi wa Ligi Kuu.
 (Guardian)

Manchester City hawatajaribu kumsajili Alexis Sanchez mwezi Januari - lakini wataangazia sana mpango wao wa kusajili beki.

Benik Afobe
Bournemouth wataiambia Crystal Palace isahau kuhusu uwepo wa uwezekano wa kumsajili Benik Afobe mwezi Januari kama majereha ya Jermain Defoe yatamfanya akae nje kwa muda mrefu.

Arsenal ni miongoni mwa klabu tatu zinazowania saini ya winga Shakhtar Donetsk, Bernard. (Express)

Meneja wa Manchester City,
 Pep Guardiola ataumia kiasi cha paundi milioni 160 kusajili wachezaji watatu kwenye majira ya joto, Alexis Sanchez, Virgil Van Dijk na Sergio Busquets wakiwa vinara kwenye orodha ya wachezaji anaowahitaji.

Swansea City watawachukua waholanzi wawili kwa kumleta Dennis Bergkamp kama sehemu ya menejimenti ya timu hiyo akiongozwa na Frank de Boer.

West Brom watamuuza beki wa kati Jonny Evans mwezi ujao kama atakataa kusaini mkataba mpya.

Arsenal wanmchunguza chipukizi wa klabu ya Barcelona, Jose Arnaiz na wanaweza kupeleka ofa ya kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Cameron Carter-Vickers 
Tottenham wanafanya mpango wa kumrejesha Cameron Carter-Vickers kutoka Sheffield United alikokuwa kwa mkopo. (Star)

Liverpool watajaribu kumsajili nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar, ambaye anakdiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 90 mwezi Januari, wakiwa kwenye mikakati ya kumaliza Ligi katika nne bora, na kuipiku Arsenal kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Mfaransa huyo.

Liverpool iko kwenye ushindani mkubwa na Borussia Dortmund kuwania saini ya beki wa klabu ya FC Basel, Manuel Akanji.

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anatarajiwa kuimarisha kikosi chake kwa kuongeza mshambuliaji mwingine mwezi Januari.

Meneja wa Norwich, Daniel Farke yuko kwenye wakati mgumu kufuatia tuhuma za kuwafanyisha wachezaji wake mazoezi magumu. (Independent)

Klabu ya Bari ya Italia inamtaka kiungo wa Celtic, Liam Henderson mwezi Januari.

Tommy Wright anasema kwamba Rangers inamtaka Michael O'Halloran arejee mwezi ujao kutoka St Johnstone alikokuwa kwa mkopo.

Roberto Mancini amewaweka sokoni wachezaji watano wa Zenit St Petersburg akitazamia kuboresha kikosi chake kuelekea mcheza wa Ligi ya Europa League dhidi ya Celtic mwezi Februari. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 22 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 22 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/22/2017 08:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.