Loading...

Zanzibar yatinga Fainali Chalenji baada ya kuichakaza Uganda bao 2-1


Zanzibar wamefuzu kwa fainali ya ubingwa wa kanda ya Afrika mashariki na kati, maarufu kama Cecafa Senior Challenge baada ya kuwalaza Uganda Cranes 2-1.

Zanzibar Heroes sasa watakutana na Kenya kwenye fainali Jumapili.

Zanzibar walifunga mwanzo kupitia Abdul Azizi Makame dakika ya 25 kisha Derrick Nsibambi akatuliza kimiyani bao la Uganda la kusawazisha naye Mohammed Issa Juma akapachika wavuni bao la pili la Zanzibar .

Ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kufika fainali michuano hiyo tangu 1995, mwaka ambao walitwaa ubingwa.

Wenyeji Kenya walifuzu baada ya kuwashinda Burundi kwa bao la muda wa ziada lililofungwa na kiungo wa kati Whyvonne Isuza.

Katibu mtendaji wa baraza la taifa la michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee tayari amesema: "Sasa Fifa wapende wasipende watatutambua."

Zanzibar si wanachama wa Fifa licha ya kupigana kwa muda mrefu watambuliwe kwa pamoja hujumuishwa na Tanzania bara.

Lakini Ali asema ndugu mkubwa hawapi fungu lao kutoka Fifa.

"Nitasema hapo tumefinywa lakini tutafanikiwa siku moja."

CAF pia haikitambui chama cha kandanda cha Zanzibar.

"Walijaribu kutuzuia CAF tusishiriki michuano hii ya Cecafa lakini ndugu mkubwa akatutetea tena tuliwaambia sisi ni baadhi ya waanzilishi miaka hiyo ikiwa Gossage Cup," asema Ali.
Zanzibar yatinga Fainali Chalenji baada ya kuichakaza Uganda bao 2-1 Zanzibar yatinga Fainali Chalenji baada ya kuichakaza Uganda bao 2-1 Reviewed by Zero Degree on 12/15/2017 07:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.