Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 15 Decemba, 2017

David Luiz
David Luiz amefanya mazungumzo na meneja wa Chelsea, Antonio Conte na kumtaka Muitaliano huyo amrejesha katika nafasi yake ya siku zote na kama atashindwa kufanya hivyo ataondoka.

Nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, ambaye anawindwa na klabu ya Manchester United ameambiwa na meneja wa klabu hiyo, Diego Simeone kuwa yuko huru kuondoka.

Klabu ya West Ham ina mpango wa kuwasajili nyota wawili wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere na Olivier Giroud.

Kiungo wa kati wa England, Jack Wilshere amethibitisha kwamba bado anasubiri kufahamishwa na Arsenal ni lini mazungumzo kuhusu mkataba wake yataanza.

Kwa mujibu wa taarifa za nchini Spain, Gareth Bale amekamilisha makubaliano yake ya awali na klabu ya Manchester United kuhusu kuondoka Real Madrid katika kipindi cha majira ya joto. (Express)

Inasemekana Pep Guardiola atahakikisha anafanikiwa kusajili beki wa kati mwezi ujao, huku Virgil van Dijk na Jonny Evans wakiwa vinara kwenye orodha yake.

Chelsea huenda wakamtumia mshambuliaji wa Belgium, Michy Batshuayi kama chambo kwenye ofa ya kumnasa winga wa klabu ya Monaco na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Thomas Lema, ambaye amekuwa akiwaniwa na Liverpool na Arsenal.

Daley Blind
Klabu ya Barcelona imeripotiwa kuwa na nia ya kumsajili nyota wa Manchester United, Daley Blind.

Aliyekuwa nyota wa klabu ya Barcelona na mshindi wa Kombe la Dunia 2002, Ronaldinho anataka kujiunga na Seneti ya Brazil. (Sun)

Jose Mourinho yuko tayari kumuuza Henrikh Mkhitaryan kwenye majira ya joto - kufanikisha mipango ya kumsajili Mesut Ozil kama mbadala wake.

Matumani ya klabu ya Liverpool kumsajili beki wa Lazio, Stefan de Vrij yameongezeka baada ya Barcelona kuonesha haina nia ya kumsajili tena.

Klabu ya Real Betis ina nia ya kumrejesha Jese Rodriguez kutoka Stoke City kwa mkopo - nyota huyo amekuwa nje ya kikosi baada ya kurejea nchini Uhispania kuwa karibu mtoto wake mchanga anayeumwa.

Meneja wa Everton, Sam Allardyce
Aston Villa wataanzisha mazungumzo na klabu ya Manchester United kuhusiana na kumfanya golikipa anayeitumikia klabu hiyo kwa mkopo, Sam Johnstone asaini mkataba wa kudumu. (Mirror)


Sam Allardyce amekiri kwamba maamuzi kuhusu future ya Ross Barkley yako juu ya uwezo wake na kudai kwamba uongozi wa Everton ndio utaamua kama nyota huyo ataendelea kukaa hadi zaidi ya mwezi Januari.

Meneja wa wa Crystal Palace, Roy Hodgson amemuonya mshambuliaji wake, Christian Benteke kwamba hawezi kuwa na mashabiki kwenye timu kama haongeza bidii, Cystal Palace inapojaribu kupanda juu kwenye jedwali la msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester United wamehoji taarifa za kiungo wa klabu ya Chelsea, Willian lakini Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza hawako tayari kumuuza mwezi Januari.

Sheffield Wednesday wanakaribia kukamili uhamisho straika wa klabu ya Manchester United, James Wilson kwa mkopo.

Kwa mujibu wa Harry Winks, klabu ya Tottenham lazima ijidhihirishe kwamba ni timu inayoweza kusimama bila 'Harry Kane'.

Everton na West Ham ni miongoni mwa timu zinazoonyesha nia ya kumsajili beki wa klabu ya Lille, Adama Soumaoro. (Daily Mail)

Meneja wa City Pep Guardiola pia atarudi sokoni kumtafuta beki wa kushoto mwezi Januari. (Manchester Evening News)

Arsenal wanakumbana na matatizo zaidi kwenye mikataba ya wachezaji wao baada ya kushindwa kufikia makubaliano na nyota na Aaron Ramsey pamoja na  Danny Welbeck juu ya mikataba mipya, ambapo mikataba yao inategemewa kuisha kwenye majira ya joto mwaka 2019.

Manchester City watajaribu kumsajili nyota wa klabu ya Real Sociedad, Inigo Martinez kama watashindwa kumnasa Virgil van Dijk na mabeki wengine wanaowahitaji. (Times)

Ripoti zinadai, karibu asilimia 58 ya wachezaji wa Ligi Kuu ya Shirikisho la soka FA ya wanawake ina mpango wa kuondoka kwa sababu za kifedha, ikiwa asilimia 88 wanalipwa chini ya paundi 18,000 kwa mwaka. (Telegraph)

Jose Mourinho akizungumza na Henrikh Mkhitaryan
Henrikh Mkhitaryan ataomba kufanya mazungumzo na Jose Mourinho kuhusiana na mstakabali wa maisha yake katika klabu ya Manchester United.

Danny Rose anasema kwamba Spurs iko tayari kuvunja tena rekodi ya klabu ya Manchester City ya kutokufungwa. (Star)

Klabu ya Rangers inatarajia kumkosa kiungo wake, Graham Dorrans kwa karibu miezi mitatu.

Morocco wameachana na mpango wa kucheza mechi ya kirafiki na Scotland kabla ya Kombe la Dunia kuanza mwakani kwa sababu mfumo wake haulingani na Spani na Ureno, ambazo watakabiliana nazo kwenye kipindi cha majira ya joto Urusi. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 15 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 15 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/15/2017 07:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.