Loading...

Diwani wa kata ya Kiwalani amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar


DIWANI wa Kata ya Kiwalani, Mussa Kafana (CUF), amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, baada ya kumshinda mpinzani wake Mariam Lulida (CCM), huku akifi kishwa ukumbini kwa kubebwa akidaiwa kuwa mgonjwa.

Uchaguzi huo ulifanyika jana Dar es Salaam baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CCM, katika kikao cha Baraza la Jiji ambapo mgombea huyo wa CUF alifikishwa ukumbini akiwa amebebwa kwa madai kwamba alikuwa anaumwa.

Akimtangaza mshindi huyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana alisema wapiga kura walikuwa 22, kura zilizopigwa zilikuwa 22 na hakuna kura iliyoharibika. Alisema baada ya uchaguzi huo, Kafana alipata kura 12 na Lulida kura 10 ikiwa ni tofauti ya kura mbili na hivyo kumtangaza Kafana kuwa mshindi wa kiti hicho.

Awali kulikuwa na mvutano kutokana na mgombea huyo wa CUF kutofika katika uchaguzi kwa madai kwamba, alikuwa mgonjwa lakini madiwani wa upinzani waligoma kujiorodhesha hadi mgombea wao afikishwe ukumbini.

Hata hivyo, pamoja na Meya wa Jiji hilo, Issaya Mwita, kusisitiza kwamba mgombea huyo ni mgonjwa, bado hali haikuwa shwari na hivyo, kulazimika kuamuru mgonjwa huyo kuletwa hali iliyofanya alifikishwa hapo akiwa amebebwa.


Mgombea huyo alipofikishwa alilazwa moja kwa moja kwenye kiti huku baadhi ya wajumbe wakionesha hali ya masikitiko kwa alichofanyiwa mgonjwa huyo na kuomba muongozo wa kuahirishwa kwa kikao hicho.

“Limefanyika kosa kubwa sana kumleta mtu huyu hapa na menejimenti ifanye utaratibu wa kumpeleka hospitali sasa hivi... na baada ya kuona hali hii naomba kikao hiki kiahirishwe tukifanye siku nyingine,” alisema Mwita.

Kutokana na hilo, Meya aliahirisha mkutano huo na mgonjwa kuamriwa kupelekwa hospitali lakini baada ya mgonjwa kutolewa nje ya ukumbi, Mkurugenzi wa Jii alisimama na kutaka kikao kiendelee na uchaguzi ufanyike kwa madai kwamba akidai imetimia.

Baada ya madiwani wa Ukawa kusikia hivyo walimbeba tena mgonjwa wao na kumrudisha ukumbini ambapo alisaidiwa kupiga kura na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea baada ya kikao hicho kuafiki.

Hata hivyo, baada ya matokeo kutangazwa Lulida aliibuka mshindi kwa zaidi ya kura mbili na ndipo alipochukuliwa kwa mara nyingine kwa madai ya kupelekwa hospitali. Alisema amesikitishwa na mvutano usiofurahisha kwa kuwa wote ni binadamu na ni kitu kimoja.
Diwani wa kata ya Kiwalani amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar Diwani wa kata ya Kiwalani amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar Reviewed by Zero Degree on 1/04/2018 03:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.