Loading...

Kikosi cha Yanga kitakachoshiriki Klabu Bingwa Afrika msimu huu


Klabu ya soka ya Yanga imetangaza kikosi chake kitakachoshiriki klabu bingwa Afrika (CAF Champions) msimu huu. Yanga inashiriki kupitia tiketi yake ya kuwa bingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2016/17.

Kikosi hicho kina jumla ya wachezaji 27 pamoja na benchi la ufundi lenye watu saba chini ya kocha mkuu George Lwandamina.

Katika kikosi hicho makipa ni Youthe Rostand, Benno Kakolanya na Ramadhani Kabwili. Walinzi wa pembeni ni Juma Abdul, Hassan Hamis, Gadiel Michael na Haji Mwinyi. Walinzi wa kati ni Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Andrew Vicent, Abdalah Shaibu na Festo Kayembe.

Viungo ni Papy Kabamba, Raphael Daud, Pato Ngonyani, Thabani Kamusoko, Pius Buswita na Said Juma. Mawinga ni Juma Mahadhi, Emmanuel Martin, Said Mussa na Geoffrey Mwashiuya.

Washambuliaji ni Amissi Tambwe, Obrey Chirwa, Yusuf Mhilu, Ibrahim Ajib, Donald Ngoma, Yohana Mkomola na Matheo Anthony.

Benchi la ufundi linaongozwa na kocha mkuu George Lwandamina, makocha wasaidizi Shadrack Nsanjigwa na Noel Mwandila, Daktari wa timu Edward Bavu, Kocha wa viungo Jacob Onyango, Meneja vifaa Mahamood Omar na Hafidh Omary.

Klabu ya Yanga SC msimu uliopita ilitupwa nje ya michuano hiyo na klabu ya Zanaco ya Zambia. Katika mchezo wa kwanza Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 kwenye uwanja wa taifa kabla ya kutoka suluhu ugenini na kutolewa kwa sheria ya bao la ugenini.
Kikosi cha Yanga kitakachoshiriki Klabu Bingwa Afrika msimu huu Kikosi cha Yanga kitakachoshiriki Klabu Bingwa Afrika msimu huu Reviewed by Zero Degree on 1/02/2018 07:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.