Loading...

Kocha wa Tanzania Prisons na Golikipa wa Mbeya City wafungiwa na TFF


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imemfungia Golikipa wa timu ya Mbeya City, Owen Chaima kucheza mechi nne sambamba na faini, baada ya kukiri kumpiga Mshambuliaji wa Azam Fc Yahya Mohamed katika mchezo uliochezwa Oktoba 27 mwaka jana kwenye uwanja wa Chamanzi Jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo umetangazwa leo na TFF baada ya kamati hiyo kuketi Januari mosi, 2018 ambapo ilipitia ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 ambapo Meneja wa Tanzania Prisons, Erasto Ntabahani alipelekwa kwenye kamati hiyo kwa kosa la kumshambulia kwa maneno muamuzi wa akiba.

Na ule kati ya Azam Fc na Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017 ambapo Mlinda Mlango wa Mbeya City Chaima alidaiwa kumpiga mshambuliaji wa Azam Fc Mohamed.

Pia, kamati ya Nidhamu imemfungia Meneja wa Tanzania Prisons, Ntabahani miezi miwili sambamba na kulipa faini kwa mujibu wa kanuni ya 40 (2) ya udhibiti wa viongozi baada ya kamati kujiridhisha kuwa Ntabahani alimshambulia kwa maneno muamuzi huyo wa akiba.
Kocha wa Tanzania Prisons na Golikipa wa Mbeya City wafungiwa na TFF Kocha wa Tanzania Prisons na Golikipa wa Mbeya City wafungiwa na TFF Reviewed by Zero Degree on 1/04/2018 03:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.