Loading...

Diego Costa arejea Atletico Madrid kwa kishindo


Mchezaji wa zamani wa Chelsea Diego Costa aliingia kama nguvu mpya na kufunga bao dakika ya tano baada ya kuingia uwanjani mechi yake ya kwanza tangu aliporejea tena Atletico Madrid.

Costa alifungia klabu hiyo bao la tatu katika mechi ambayo walishinda 4-0 dhidi ya Lleida Esportiu hatua ya 16-bora katika michuano ya Kombe la Mfalme maarufu kama Copa del Rey.

Chelsea walikubali kumuuza Costa, 29, kwa klabu yake ya zamani ya Atletico Septemba ingawa hakuruhusiwa kucheza hadi mwezi huu.

Aliingizwa uwanjani dakika ya 64.

Diego Godin, Fernando Torres na Antonie Griezmann walifungia Atletico mabao hayo mengine.

"Nina furaha sana kuwa mchezaji tena na kuichezea tena Atletico Madrid. Ilikuwa muhimu sana kwangu," alisema.

"Singetarajia mwanzo mwingine bora kuliko huu wa kipindi cha pili cha maisha yangu hapa Atletico.

"Nilipewa fursa ya kucheza tena na nikapata fursa ya kufunga, hilo linanijaza na furaha zaidi."

Meneja Diego Simeone alisema kurejea kwa Costa kumewaongezea nguvu.

Costa ambaye ni mzaliwa wa Brazil lakini huchezea timu ya taifa ya Uhispania alijiunga na Chelsea kutoka Atletico kwa £32m mwaka 2014 na akawafungia mabao 58 katika mechi 120, 20 yakiwa kwenye Ligi ya Premia msimu uliopita ambapo aliwasaidia kushinda ligi.
Diego Costa arejea Atletico Madrid kwa kishindo Diego Costa arejea Atletico Madrid kwa kishindo Reviewed by Zero Degree on 1/04/2018 03:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.