Loading...

Mke wa Kingunge afariki dunia


MKE wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kueleza kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

“Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling’atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka,” amesema.
Mke wa Kingunge afariki dunia Mke wa Kingunge afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 1/04/2018 11:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.