Liverpool kutumia pauni milioni 100 kusajili golikipa
Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp |
Klabu hiyo haina muda wa kupoteza kuwapata wachezaji inaowahitaji. Liverpool inatarajia kupokea fedha nyingi kwa kumuuza Philippe Coutinho na tayari Jurgen Klopp ameshaamua kuzitumia fedha hizo kwa ajili ya kujipatia wachezaji wapya.
Klopp anataka kumsajili golikipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak ili achukuwe nafasi ya Simon Mignolet. Oblak alisema kwenye majira ya joto kwamba, hajui kama angeweza kubakia katika klabu hiyo ya Uhispania baada ya msimu huu. Na tangu wakati huo, Arsenal na Liverpool zote kwa pamoja zimekuwa zikiwania saini ya mchezaji huyo.
Akizungumza na Marca, Oblak alisema, “Mimi ni mchezaji wa Atletico na itaendelea kuwa hivyo hadi mwisho wa msimu. Baada ya hapo, sijui itakuwaje, tutaona. Huwezi kujua. Wakati mwingine mambo hubadilika siku hadi siku. Kwa sasa, ninaizungumzia Atletico pekee, ambako ninaishi kwa furaha.”
Liverpool pia inamfuatilia golikipa wa klabu ya Roma, Alisson na wa Stoke City, Jack Butland lakini chaguo lao la kwanza ni Jan Oblak, ambaye thamani yake ni pauni milioni 100 na taarifa zinadai kwamba Klopp anatazamia kutumia fedha atakazoingiza kwa kumuuza Philippe Coutinho kwenda Barcelona mwezi huu, kumsajili raia huyo wa Slovenia.
Golikipa wa klabu ya Atletico Madrid, Jan Oblak |

Reviewed by Zero Degree
on
1/06/2018 07:12:00 PM
Rating: