Loading...

Monaco yatangaza dau la Thomas Lemar


Monaco walikubali ofa ya pauni milioni 90 kutoka Arsenal siku ya mwisho ya usajili kwenye majira ya joto, kabla ya Lemar kukataa kuhamia Uingereza, na mabingwa hao wa Ufaransa wanasistiza kwamba mazungumzo kuhusiana na bei ya nyota huyo yataanzia hapo walipoishia.

Monaco wameona Liverpool ikipokea ongezeko la pauni milioni 30 kwenye bei ya awali kwa kumuuza Philippe Coutinho kwenda Barcelona mwezi huu na wanahisi kwamba thamani ya Lemar pia imepanda.

Msimamo mkali wa klabu ya Monaco unaweza kuikatisha tamaa Liverpool na hawako tayari kufuatilia uhamisho huo kwa sababu tu wamemuuza Coutinho kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 142 iliyovunja rekodi ya klabu.

Liverpool na Arsenal zitatakiwa kulipa kiasi cha pauni milioni 90 kumnasa Thomas Lemar kutoka Monaco.

Monaco wako tayari kumuuza Lemar mwezi huu kwa sababu wako nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na wako nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Ufaransa kwa pointi 9.

Meneja wa klabu ya Monaco, Leonardo Jardim
Meneja wa klabu hiyo, Leonardo Jardim amefungua milango kwa Lemar kuondoka Monaco, akidai “mambo mengi yanaweza kutokea”.

Jardim alisema: “Hatuna utaratibu wa kuuza wachezaji katikati ya msimu. Lakini mwezi ni mkubwa sana na mambo mengi yanaweza kutokea.”

Thomas Lemara akiwa Timu ya Taifa
Lemar, mwenye umri wa miaka 22, alifanya vizuri wakati Monaco ikitwaa taji la Ligue 1 katika mazingira magumu na kisha klabu yake kupoteza nyota wengi kwenye kipindi cha majira ya joto. Msimu huu ameshafunga magoli manne na kutoa 'assist' nne kwa klabu na Timu yake ya Taifa.
Monaco yatangaza dau la Thomas Lemar Monaco yatangaza dau la Thomas Lemar Reviewed by Zero Degree on 1/09/2018 07:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.