Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Januari, 2018

Paulo Dybala
Paris Saint-Germain imejiondoa kwenye kinyan'ganyiro cha kuwania saini ya mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala, na kuipa uhuru wa kutosha klabu ya  Manchester United.

Klabu ya Arsenal imemweka Thomas Lemar mstari wa mbele kwenye orodha ya wachezaji inaowahitaji na iko tayari kuishawishi Monaco imuuze nyota huyo mwezi Januari.

Chelsea, Manchester United na Arsenal kushindania saini ya winger wa klabu ya Bayer Leverkusen, Leon Bailey kwenye majira ya joto.

Rafa Benitez amefunga milango kwa mchezaji yeyote anayetaka kuondoka Newcastle mwezi huu ili kuinusuru klabu isishuke daraja, akiwemo Jonjo Shelvey anayewindwa na klabu ya West Ham pamoja na Aleksandar Mitrovic, ambaye anawindwa na Brighton.

West Ham wana fanya mpango wa kumnasa kiungo wa Arsenal, Francis Coquelin lakini uwezekano wa kumpata ni mdogo sana baada ya Valencia kutoa ofa ya pauni milioni 12. (Mirror)

Sergio Ramos
Sergio Ramos amemtaka Florentino Perez kufanya usajili wa wachezaji wapya wenye uwezo mkubwa ili kuiwezesha klabu ya Real Madrid kutwaa Taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa.

Florentino Perez ana mpango wa kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha Real Madrid, kumpa nafasi Zinedine Zidane kuanza kupanga Timu mpya ambayo itakuwa na ngvu zaidi. (Don Balon)

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez anaweza kukamilisha taratibu za kuhamia Manchester City mwishoni mwa wiki hii.

Francis Coquelin na Mathieu Debuchy wanatarajiwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaoakiwa kuondoka katika klabu ya Arsenal mwezi huu. (ESPN)

Aliyekuwa nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo anatazamia kurejea kwenye Ligi Kuu ta Uingereza, huku akihusishwa kujiunga na klabu zaidi ya moja katika Ligi hiyo maarufu Duniani kote.

Manchester City inaandaa ofa ya pauni milioni 50 kwa ajili ya uhamisho wa beki wa klabu ya  Leicester, Harry Maguire. (Manchester Evening News)


Manchester City wameanza mkakati wao wa kwanza kumnasa Alexis Sanchez kutoka Arsenal na ofa yao ya pauni milioni 30 inaweza kukamilisa taratibu zote za uhamisho wa nyota huyo.

Jose Mourinho bado ana hasira kufuatia bodi ya klabu ya Manchester United kumlazimisha achague nani wa kumsajili kati ya Nemanja Matic na Ivan Perisic kwenye majira ya joto.

West Ham wanakaribia kumsajili kiungo wa Newcastle, Jonjo Shelvey kwa dau la pauni milioni 12.

Yerry Mina
Klabu ya Barcelona inatarajiwa kutangaza usajili mpya, huku beki wa Timu ya Taifa ya Colombia, Yerry Mina akijiandaa kujiunga na vigogo hao akitokea Palmeiras. (Express)

Matumaini ya klabu ya Chelsea kutaka kumsajili beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro yamekufa baada ya klabu hiyo kupandisha bei ya nyota huyo hadi pauni milioni 80.

Derby County wameanzisha mazungumzo  juu ya mkataba mpya na meneja anayewindwa na klabu ya Stoke City, Gary Rowett. (Telegraph)

Stoke City watalazimika kusubiri hadi msimu ujao ikiwa wanataka kumwajiri aliyekuwa meneja wa West Ham, Slaven Bilic kama meneja wao mpya.

Leicester wako tayari kumuuza mshambuliaji wao Kelechi Iheanacho kwa bei ya hasara ikiwa watampata mnunuzi atakayekuwa tayari kutoa pauni milioni 25 mwezi huu.

Mshambuliaji wa Newcastle, Aleksandar Mitrovic ameanza mazungumzo na klabu ya Bordeaux ya Ufaransa. (Sun)

Klabu ya Bournemouth inatarajiwa kutumia pauni milioni 1 kumsajili straika wa Colchester United, Sammie Szmodics.

Schalke 04 hawataruhusu mazunguzo kuhusiana na uhamisho wa Leon Goretzka yafike mwisho wa mwezi Januari.

Kwa mujibu wa ripoti za Uhispania, Real Madrid wamekata tamaa ya kufanikisha uhamisho wa beki wa klabu ya Chelsea, Marcos Alonso. (Star)

Mathieu Debuchy
Arsenal wanaweza kumtoa Mathieu Debuchy kwa West Brom kama sehemu ya ofa yao kumnasa Jonny Evans. 
(Daily Mail)

Everton wako tayari kumuuza Oumar Niasse kwa pauni milioni 13, na kuanzisha vita kati ya Crystal Palace, West Brom na West Ham, ambapo zote zimekuwa zikihusihwa na kuwania saini ya nyota huyo. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/09/2018 11:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.