Loading...

Mwalimu anashikiliwa kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi mlemavu


Mwalimu mmoja wa shule ya wanafunzi wenye ulemavu katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, amefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mwanafunzi mwenye ulemavu na kumsababishia ujauzito.

Akizungumza katika kongamano la wadau wa elimu lililoandaliwa na shirika la TCRS, Mkuu wa wilaya Kilwa, Christopher Ngubiagai, amesema kitendo kilichofanywa na mwalimu huyo sio cha kukifumbia macho huku mwanafunzi akiwa amekatisha kuendelea na masomo yake.

Mkuu huyo wa wilaya pia, akaeleza wilaya yake inavyoathirika na tatizo la tatizo la mimba za utotoni na utoro na kupelekea kufanya vibaya katika mitihani ya Kimkoa na Kitaifa.

Wilaya hiyo imeshika nafasi ya sita kati ya wilaya sita za mkoa wa Lindi katika matokeo ya mithani wa darasa la Saba mwaka jana, huku ikishika nafasi ya 160 Kitaifa.
Mwalimu anashikiliwa kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi mlemavu Mwalimu anashikiliwa kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi mlemavu Reviewed by Zero Degree on 1/25/2018 12:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.