Loading...

Mzee Akilimali ajitosa sakata la Chirwa, ...adai wakulaumiwa ni kocha

Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa akisindikizwa na askari alipowasili na wanzake kutoka Zanzibar
MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amemtetea mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Obrey Chirwa kufuatia kukosa penati katika mechi ya juzi dhidi ya URA ya Uganda kwenye Kombe la Mapin­duzi.

Yanga iliondolewa katika nusu fainali kwa penalti 5-4, ambapo Chirwa alikosa penati ya mwisho kwa upande wa Yanga na kusaba­bisha gumzo baada ya tukio hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali
Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Championi, Mzee Akilimali alisema kwamba, Chirwa hakufan­ya makosa katika kupiga penati ya mwisho kwani alidhamiria kufunga na kilichotokea ni bahati mbaya na kuongeza kuwa, kocha ndiye anayepaswa kulaumiwa kutokana na kumtumia licha ya kutokuwa na ma­zoezi ya pamoja na wenzake.

“Yanga tumetolewa kiume katika michuano ya Mapinduzi kwani hadi tunatoka tumefanikiwa kufanya vyema hadi dakika 90 lakini kili­chotokea hakipaswi kulaumiwa mchezaji.

“Timu ilicheza vizuri ilipamba­na na hatimaye kuweza kufikia hapo tulipofikia na ilikuwa ni lazima timu moja isonge mbele.

“Siwezi kumlaumu Chirwa, kilichotokea ni bahati mbaya kwani, hata wachezaji wa­zuri Ulaya wanakosa penalti sembuse yeye, anayepaswa kulaumiwa ni kocha kwanini amemchezesha mchezaji akiwa hana mazoezi, naona anayarudia yaleyale ya Kocha Hans Pluijm,” alisema Akilimali.
Mzee Akilimali ajitosa sakata la Chirwa, ...adai wakulaumiwa ni kocha Mzee Akilimali ajitosa sakata la Chirwa, ...adai wakulaumiwa ni kocha Reviewed by Zero Degree on 1/12/2018 01:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.