Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 12 Januari, 2018

Riyad Mahrez (Leicester City)
Liverpool wameanza mazungumzo na klabu ya Leicester juu ya uhamisho wa Riyad Mahrez, lakini kwa upande wake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema anataka kujiunga na Arsenal.

Meneja wa klabu ya Leicester, Claude Puel anaamini mchezaji mpya aliyesajiliwa na klabu hiyo, Fousseni Diabate atakuwa kama Riyad Mahrez.

Crystal Palace wanakaribia kukamilisha taratibu za uhamisho wa golikipa wa klabu ya Getafe, Vicente Guaita. (Express)

Real Madrid wana mpango wa kusajili beki atayesaidiana na Sergio Ramos, huku majina kama Leonardo Bonucci (AC Milan), David Luiz ( waChelsea) na Aymeric Larpote ( wa Athletic Bilbao) yakitajwa kwenye orodha ya meneja wa klabu hiyo, Zinedine Zidane. (Don Balon)

Manchester United imetoa ofa ya pauni milioni 25 kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa Taifa la Chile na Arsenal, Alexis Sanchez. (Guardian)

Kevin De Breyne anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Manchester City utakomwingizia pauni 200,000 kwa wiki. (Manchester EveningNews)

Manchester United wamepunguza kasi ya kuwania saini ya Alexis Sanchez na kuelekeza nguvu kwa Jamie Vardy pamoja na Javier Hernandez.

Arthur Melo
Manchester United na Chelsea zinatarajiwa kushindania saini ya Mbrazil, Arthur Melo kutoka Gremio.

John Hall anahofia 'future' ya Newcastle kama mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley hataiuza hivi karibuni.

Kiungo wa Crystal Palace, James McArthur amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo.

Meneja wa Bournemouth, Eddie Howe anamfuatilia beki wa Denmark, Mads Pedersen.

Klabu ya Sunderland iko kwenye mazungumzo na Burnley kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo, Jon Walters.

Meneja wa klabu ya Reading, Jaap Stam ana mpango wa kusajili nyota wawili, mmoja akiwa mshambuliaji wa Barnsley, Tom Bradshaw na wapili ni beki wa Southampton, Sam McQueen.

QPR na Bolton kwa wakati mmoja zimejikuta zikitaka kumsajili winga wa klabu ya Cardiff, Anthony Pilkington. (Star)

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy anaamini kwamba hakuna mchezaji yeyote wa muhimu atakayeondoka Spurs kwenye majira ya joto.

Francis Coquelin
Francis Coquelin amekamilisha taratibu za uhamisho wake kwenda Valencia baa ya kuitumikia klabu ya Arsenal kwa karibuni muongo mmoja. (90min)

Stoke City wamempa Quique Sanchez Flores ofa ya kazi ya umeneja na wako wanasubiria majibu kutoka kwake.

Klabu ya Everton inajiandaa kuwasilisha ofa ya pauni milioni 20 ili kumnasa winga wa Arsenal, Theo Walcott.

Meneja wa Nottingham Forest, Aitor Karanka anafanya mpango wa kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Charly Musonda. (Telegraph)

Jose Mourinho na Antonio Conte wana mgogoro mkubwa kati yao, huku wote wakiwa kwenye orodha ya mameneja wanaowaniwa na klabu ya PSG.

Julian Draxler (katikati) alipokwenda kushuhudia mechi ya NBA mjini London
Mashabikiwa Arsenal wameshawishika kwamba, mshambuliaji wa PSG, Julian Draxler anajiunga na klabu yao baada ya kuonekana kwenye mchezo wa NBA mjini London akiwa na wachezaji kadhaa wa klabu hiyo ya EPL.

Liverpool na Tottenham kushindania saini ya nyota wa klabu ya Norwich, James Maddison kwenye majira ya joto.

Leicester wamethibitisha kwamba, Kelechi Iheanacho hataondoka katika klabu hiyo mwezi huu. (Mirror)

Amanda Staveley anakumbana na ushindani mkubwa kwenye ununuzi wa klabu ya Newcastle baada ya matajiri wa Dubai kutoa ofa ya kutaka kuinunua klabu hiyo.

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu, huku Max Allegri na Luis Enrique wakiwa kwenye orodha ya wanaotarajiwa kuchukua nafasi yake.

Mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge
Liverpool wako tayari kumuuza mshambuliaji wao, Daniel Sturridge kwa pauni milioni 30 baada ya nyota huyo kuomba kuondoka Anfield. (Daily Mail)

Alexis Sanchez ametupilia mbali ofa ya Jose Mourinho na badala yake anataka kuhamia Manchester City.

Theo Walcott hajui kama ataruhusiwa kuonoka Arsenal mwezi Januari, Licha ya kwamba klabu za Everton na Southampton zimeonyesha nia thabiti ya kutaka kumsajili.

Cardiff watalipia kiasi cha pauni milioni 2 kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Bolton, Gary Madine.

Reading wako kwenye mazungumzo na klabu ya Derby kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo, Chris Martin kwa mkopo. (Sun)

Manchester United ina mpango wa kumsajili kiungo klabu ya Shakhtar Donetsk,  Fred (raia wa Brazil), ambaye pia anawindwa na Pep Guardiola (Record).

Alexis Sanchez anategemewa kujiunga na Manchester City mwezi huu, licha ya kwamba klabu ya Manchester United imejitokeza mwishoni na ofa mezani.

Liverpool wanafanya mawasiliano rasmi na klabu ya RB Leipzig, wakiwa na mpango wa kumleta mshambuliaji, Naby Keita achue nafasi iliyoachwa na Philippe Coutinho. (Times)

Sanchez angependelea kuhamia Manchester City, lakini klabu hiyo inataka kumsajili mchezaji huyo kwa pauni 20 tu, kiasi ambacho Arsenal haiko tayari kupokea.

Beki wa klabu ya Swansea, Alfie Mawson
Meneja wa klabu ya Swansea, Carlos Carvalhal anasema kwamba, klabu yoyote ambayo itataka kumsajili beki wake, Alfie Mawson italazimika kulipa dau la pauni milioni 50. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 12 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 12 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/12/2018 12:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.