Loading...

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine

Alphayo Kidata
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Januari 11, 2018 amefanya uteuzi na kuwateua Bw. Alphayo Kidata pamoja na Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi kuwa mabalozi wa nchi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Alphayo Kidata umeanza tarehe 10 Januari, 2018 na kabla ya uteuzi huo, Bw. Alphayo Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Mabalozi Mabalozi hao wateule watapangiwa vituo vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika.
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Reviewed by Zero Degree on 1/11/2018 06:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.