Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Januari, 2018

Dele Alli
Tottenham wameanzisha mazungumzo juu ya mkataba mpya na Dele Alli, huku kukiwa na tetesi zinazomhusisha nyota huyo na uhamisho kwenda klabu kadhaa za Ulaya ikiwemo Real Madrid na PSG.

Meneja wa Bournemouth, Eddie Howe anataka kumchukuwa chipukizi wa klabu ya Chelsea, Charly Musonda mwezi huu.

West Ham imeambiwa kwamba, inatakiwa kulipa kiasi cha pauni milioni 15 kumpata nyota wa klabu ya Bournemouth, Harry Arter.

Burton Albion wanafanya mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Derby, Darren Bent kwa mkopo.

Swansea wanasita kukubaliana na bei ya Ryan Federick kutoka Fulham, mbapo klabu hiyo inataka dau la pauni milioni 5. (Mirror)

Arsene Wenger amehamishia nguvu yake kubwa kwa mshambuliaji wa klabu ya Bordeaux, Malcom anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 45, anataka aje kuchukua nafasi ya Alexis Sanchez.

Wachezaji wa Manchester City wanategemea Alexis Sanchez atakuwa mchezaji mwenzao kabla mwezi huu haujaisha.

Liverpool inataka kumbakisha Roberto Firmino na kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wao wa muhimu. (Times)

Nyota wa Klabu ya West Ham, Diafra Sakho
Crystal Palace wamefikia makubaliano na klabu ya West Ham juu ya ada ya uhamisho wa nyota wa klabu hiyo, Diafra Sakho, na atatarajiwa kufanyiwa vipimo siku chache zijazo. (Sky Sports)

Guangzhou imekanusha taarifa zinazodai kwamba ina itashindana na wapinzani wao kwenye Ligi Kuu ya China, Beijing Guoan kuwania saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortimund, Aubameyang. (ESPN

Jose Mourinho anamnyima usingizi rais wa klabu ya Real Madrid baada ya kujitokeza na ofa ya kutaka kumsajili Marco Asensio. (Don Balon)

Manchester United wanafikiria kuhusu umuhimu wa dili la pauni milioni 13 kwa winga wa klabu ya PSG, Lucas Moura, ambaye mawakala wake wanakazania kufanikisha uhamisho wake kwenda klabu yoyote kubwa kati ya nne zilizo bora kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Independent)

Quique Sanchez Flores yuko mstari wa mbele kupewa kibaru cha kuinoa Stoke City, huku klabu hiyo ikiendelea kufikiria kumshawishi Martin O'Neill.

Klabu ya West Ham imetoa ofa ya pauni milioni 19 kwa ajili ya kiungo wa Anderlecht, Leander Dendoncker.

Roy Hodgson anasema kwamba, idadi kubwa ya majeruhi katika klabu ya Crystal Palace, itaichochea klabu yake kuongeza juhudi ya kusaka wachezaji wapya mwezi huu.(Express)

Klabu ya Liverpool inataka kumpa ofa ya makataba mpya mshambuliaji wake, Roberto Firmino ambao utamfanya abaki Anfield kwa muda wote uliosalia katika maisha yake ya soka. (Telegraph)

Brendan Rodgers hana haraka ya kuvunja rekodi ya usajili katika klabu ya Celtic kwa kumnasa mshambuliaji Odsonne Edouard anayeichezea klabu hiyo kwa mkopo akitokea PSG.

Jonny Evans
Jonny Evans anapima uzito kabla ya kufanya maamuzi baada ya Manchester City na Arsenal kupeleka ofa West Brom.(Daily Mail)

Manchester City wataanzisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya na Raheem Sterling ambao umfanya alipwe pauni 250,000 kwa wiki. (Guardian)

Olivier Giroud atabaki Arsenal na kupigania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza, akiwa na lengo la kwania nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Ufaransa kwenye Kombe la dunia.

Arsenal watamruhusu Alexis Sanchez aondoke kama watafanikiwa kupata mtu atakayechukua nafasi yake, huku Arsene Wenger akifanya mipango ya kumnasa Cristian Pavon kutoka Boca Juniors.

Islam Slimani ndio tumaini la Aston Villa kufanikisha uhamisho wa mshambuliaji wa Leicester, Leonardo Ulloa kwa mkopo, huku meneja wa klabu hiyo, Claude Puel akionekana kutokuwa tayari kuwaachia wote wawili waondoke mwezi januari.

Carlton Cole anafanya mazoezi na AFC Wimbledon, huku klabu ya Milton Keynes Dons ikiwa na matumaini ya kufanikiwa kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza. (Sun)

Mshambuliaji wa Watford, Stefano Okaka anaweza kujiunga na Marseille baada ya pendekezo la kuungana kwa mara nyingine tena na Walter Mazzarri katika klabu ya Torino kushindikana.

Rafinha
Arsenal inataka nyota wa klabu ya Barcelona, Rafinha aje Emirates kuchukua nafasi ya Mesut Ozil.

Klabu ya Millwall imempa mkataba wa miaka miwili beki wao wa muda mrefu, Tony Craig.

Norwich inamtaka beki wa Ado Den Haag, Tyronne Ebuehi kama mtu sahihi anayefaa kuchukua nafasi ya Russell Martin, ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya Rangers. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/11/2018 12:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.