Loading...

Rais Magufuli amjulia hali Mzee Kingunge (Picha)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amelazwa akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kujeruhiwa na Mbwa wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Januari, 2018 amewajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam wakiwemo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti.

Katika wodi ya Mwaisela, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa wake, nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Dkt.Ibrahim Mkoma anayemuhudumia Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngambale Mwiru ambaye amaelazwa katika Wodi ya Mwaisela hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambapo akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kujeruhiwa na Mbwa wake.
Dkt. Ibrahim Mkoma wa hospitali hiyo amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Mzee Kingunge inaendelea vizuri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfunika shuka Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngambale Mwiru alipomtembelea kumjulia hali katika Wodi ya Mwaisela hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambapo amelazwa akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kujeruhiwa na Mbwa wake.
Mzee Kingunge amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kumuona hospitalini hapo na amemueleza kuwa sasa anajisikia nafuu baada ya kupata matibabu.

Pamoja na kumpa pole na kumuombea apone haraka Mhe. Rais Magufuli amesema anatambua mchango mkubwa wa Mzee Kingunge katika siasa na maendeleo ya nchi.

Katika wodi ya Sewahaji, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Bw. Richard Kajumulo ambaye ni Kaka wa Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Bw. Said Abeid Salim, Bi. Amina Ismail Shirwa, Mzee Hamad Lila na amempa pole Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula aliyefiwa na Mama yake mzazi wakati Mhe. Rais akiwa wodini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Kaka wa Profesa Anna Tibaijuka ajulikanaye kwa jina la Richard Kajumulo ambaye amelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali na Profesa Anna Tibaijuka paomoja na mgonjwa ambaye ni kaka yake ajulikanaye kwa jina la Richard Kajumulo aliyelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimwagia maji ya Baraka Kaka wa Profesa Anna Tibaijuka ajulikanaye kwa jina la Richard Kajumulo ambaye amelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amewajulia hali mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa matibabu ya moyo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.
Maria na Consolata wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kuwaona na kuwapa pole na pia wameongoza sala ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi amesema matibabu kwa Maria na Consolata ambao ni wanafunzi mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Ruaha (RUCU) yanakwenda vizuri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi kuhusu hali ya watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.
Aidha, Prof. Janabi amesema taasisi hiyo imefanikiwa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa moyo 1,400 katika mwaka uliopita na kwamba inashika nafasi ya tatu barani Afrika kwa utoaji wa huduma bora za matibabu ya moyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt.Khuzeima Khanbahi Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo anayewahudumia Mapacha walioungana Maria na Consolata pamoja na Profesa Janabi mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete baada ya kuwa tembelea na kuwajulia hali hospitalini hapo Januari 6,2018.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa wanayofanya kutibu wagonjwa na amesema Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili ili kuboresha huduma zaidi.

“Nawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote, mnafanya kazi kubwa ya kuwatibu wagonjwa, pia mmeboresha hospitali na inaonekana ni safi, mimi niwaahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira yenu ya kazi ili muendelee kutoa huduma nzuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimu Manesi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi pamoja na wafanyakazi wengine wa Taasisi hiyo mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wapishi wanaofanya kazi ndani ya Hospitali ya Muhimbili wakati akitoka kuona wagonjwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Januari, 2018.
Rais Magufuli amjulia hali Mzee Kingunge (Picha) Rais Magufuli amjulia hali Mzee Kingunge (Picha) Reviewed by Zero Degree on 1/06/2018 06:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.