Loading...

Mawaziri wawili wa zamani wa Zimbabwe wakamatwa kwa tuhuma za rushwa

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa
Mawaziri wawili wa zamani wa Zimbabwe wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Samuel Undenge ambaye alikua waziri wa nishati anatuhumiwa kutumia dola elfu kumi na mbili kwa kampuni ambayo haukufanya lolote.

Walter Mzembi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje amesema tuhuma hizi ni za kisiasa
Kwa upande wa wake Walter Mzembi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati wa utawala wa Robert Mugabe aliyeondolewa madarakani mwezi Novemba, anatuhumiwa kuchangia baadhi ya mali za televisheni ya Taifa kwa kanisa moja nchini humo bila ya idhini ya serikali.

Wote wawili wamekana mashitaka hayo.Inatarajiwa kesi hizo zitasikilizwa tena baadae mwezi huu.

Rais mpya Emmerson Mnangagwa ameapa kupambana na rushwa iliyodumu karibia wakati wote wa utawala wa Robert Mugabe.

Waziri wa zamani wa nishati Samuel Undenge
Lakini wakosoaji wanasema watu wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani ni wale tu wanaohoji namna Mnangagwa aliyoingia madarakani.
Mawaziri wawili wa zamani wa Zimbabwe wakamatwa kwa tuhuma za rushwa Mawaziri wawili wa zamani wa Zimbabwe wakamatwa kwa tuhuma za rushwa Reviewed by Zero Degree on 1/06/2018 06:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.