Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 6 Januari, 2018

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham, Harry Kane
Manchester United wako tayari kuipiku klabu ya Real Madrid kwenye jaribio la kuipata saini ya kinara wa mabao Ligi Kuu ya Uingereza, Harry Kane kutoka Tottenham.

Stoke City imeionya West Ham kwamba, Joe Allen hatauzwa mwezi huu, klabu ya West Ham ikionyesha kukataa tamaa ya kuzuia kujirudia kwa kitendo cha Marko Arnautovic kuondoka klabuni.

Shaw anatarajia kubaki Manchester United hadi kufikia majira ya joto baada ya mkutano wa siri na Jose Mourinho.

Tottenham wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya Moussa Sissoko anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30.

Olivier Giroud
Besiktas wanatazamia kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud baada ya kummuza Cenk Tosun.

Newcastle wanatazamia kufanya usajili wa kushitukiza mwezi Januari kwa kumnasa golikipa wa Timu ya Taifa ya Uingereza, aliyepoteza nafasi yake kwenye kikosi cha klabu ya West Ham, Joe Hart after. (Mirror)

Liverpool wameulizia uwezekano wa uhamisho wa Luis Suarez, Philippe Coutinho akitarajiwa kuondoka Anfield kwenda Barcelona kwenye dirisha dogo la usajili mwezi huu. (Don Balon)

Liverpool wamewasiliana na Leicester City, baada ya Jurgen Klopp kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Riyad Mahrez.

Arsenal inaachana na Theo Walcott anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30, huku Southampton ikiwa mstari wa mbele kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota huyo, aliyekuwa mchezaji wao wa zamani. (Sun)

Ross Barkley
Ross Barkley amekamilisha taratibu za uhamisho kwenda Chelsea kutoka Everton kwa ada ya pauni milioni 15. (Sky Sports)

Nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard amekataa ofa ya pili ya mkataba mpya, huku klabu ya Real Madrid ikionyesha nia ya kutaka kumsajili.

Rafael Benitez anapigania kuilinda Newcastle ishuke daraja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuipa kipaumbe michuano ya FA Cup. (Star)

David Moyes amefikiria kumhakikishia Joe Hart kwamba atampa nafasi ya kufufua kiwango chake katika klabu ya West Ham kabla ya Kombe la Dunia 2018. (Guardian)

Klabu ya Newcastle ina nia ya kumsajili Danny Ings na inakaribia kukamilisha taratibu za uhamisho wa Kenedy kutokea Chelsea kwa mkopo. (Telegraph)

Philippe Coutinho anatarajia kujiunga na klabu ya Barcelona baada Liverpool kuhitaji dau la pauni milioni 145 kumruhusu nyota huyo aondoke Anfield.

Ruben Loftus-Cheek
Roy Hodgson ana matumani kwamba, klabu yake ya Crystal Palace itafanikisha usajili wa moja kwa moja wa Ruben Loftus-Cheek baada ya klabu ya Chelsea kukamilisha uhamisho wa Ross Barkley kutoka Everton.

Manchester City wanajiandaa kulipa dau la pauni milioni 35 kumnasa Alexis Sanchez baada ya kumpoteza Gabriel kwa miezi miwili. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 6 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 6 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/06/2018 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.