Loading...

Rais Magufuli ateua naibu waziri mpya

Mbunge wa Bukombe, Mh. Doto Biteko
Rais John Magufuli ameongeza baraza lake la mawaziri kwa kumteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa kufuatia uteuzi huo Wizara ya Madini sasa itakuwa na waziri na naibu mawaziri wawili.

Biteko ambaye ni Mbunge wa Bukombe na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.

Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe 08 Januari, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli ateua naibu waziri mpya Rais Magufuli ateua naibu waziri mpya Reviewed by Zero Degree on 1/06/2018 09:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.