Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 4 Januari, 2018

Thomas Lemar
Nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar amechagua kujiunga na klabu ya Liverpool kuchukuwa nafasi ya Philippe Coutinho, ambaye anatarajiwa kwenda Barcelona.

Klabu ya Ostersunds ya Sweeden inataka kumsajili kiungo wa Celtic, Liam Henderson. (Express)

Klabu ya Manchester City inatazamia kumsajili nyota wa Barcelona, Samuel Umtiti anayekadiriwa kuwana na thamani ya puni milioni 60. (ESPN)

Gary Neville anasema kwamba, kumwacha Coutinho aondoke Liverpool mwezi huu ni wazimu.

Huwezi kuwa katika kiwango cha juu kila siku, kila mchezaji ana wakati wa kupanda na kushuka - Dele Alli. (Sky Sports)

Manchester United wanahofia Jose Mourinho anaweza kujiuzulu mwishoni mwa msimu.

Meneja wa Stoke City, Mark Hughes anatarajiwa kufanya mazungumzo na bodi ya klabu huku kukiwa na mwenendo mbaya wa kikosi chake na future yake kuwa shakani katika klabu hiyo.

Tottenham wako tayari kubadili mfumo wake wa malipo kumfanya Harry Kane kuwa Muingereza anayelipwa fedha nyingi  kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa kumpa mshara wa pauni 200000 kwa wiki. (Daily Mail)

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amesema kwamba, David Luiz na Michy Batshuayi wanaruhusiwa  kuondoka mwezi Januari kama watahitaji kufanya hivyo. (Telegraph)

Watford wanamtaka kiungo wa klabu ya Sunderland, Didier Ndong, straika wa Leicester, Islam Slimani na nyota wa klabu ya Liverpool, Lazar Markovic mwezi  Januari.

Theo Walcott
Southampton, West Ham, Newcastle na Everton zote zinawania saini ya winga wa klabu ya Arsenal, Theo Walcott.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho atazuia uhamisho wa Henrikh Mkhitaryan kwenda Inter Milan. (Star)

Everton wanakaribia kukamilisha taratibu za uhamisho wa Cenk Tosun baada ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na rais wa Besiktas, Fikret Orman.

Robbie Keane
Robbie Keane anaweza kuushangaza ulimwengu kwa kurejea Wolves klabu hiyo ikikaribia kupanda daraja na kurejea Ligi Kuu ya Uingereza.

Klabu ya Chelsea iko tayari kutoa dau la pauni milioni 50 mwezi Januari kama ada ya uhamisho wa beki wa kalbu ya Juventus, Alex Sandro.

Arsene Wenger anasema kwamba, Alexis Sanchez atakuwa huru kuondoka mwezi huu endapo Arsenal itapata mtu anayefaa kuchukuwa nafasi yake.

West Brom wako tayari kumuuza Jonny Evans mwezi huu kama hatakubali kusaini mkataba mpya, huku Manchester United na Manchester City zikiwa tayari kumsajili beki huyo. (Mirror)

Danny Rose
Danny Rose yuko kwenye mipango ya uhamisho ya Manchester United, Jose Mourinho akiitaka bodi ya klabu hiyo kuhakikisha inamsajili nyota huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anamtaka winga wa klabu ya PSG, Lucas Moura kwa mkopo mwezi huu.(Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 4 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 4 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/04/2018 10:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.