Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 2 Januari, 2018

Moussa Dembele
Thierry Henry amemshauri Moussa Dembele aondoke Celtic ili apate mafanikio zaidi katika soka. (Record)

Dili la Everton kumsajili Cenk Tosun kutoka Besiktas liko hatarini kuzima baada ya pande hizo mbili kushindwa kufikia mwafaka wa makubaliano juu ya ada ya uhamisho katika mazungumzo yaliyofanyika kwa muda wa masaa 11.

Manchester United wako tayari kumtoa James Wilson kwa mkopo. (Mirror)

Besiktas wameongeza ada ya uhamisho wa Cenk Tosun hadi pauni milioni 27 baada ya Everton kupeleka ofa.

Samuel Umtiti
Barcelona wako tayari kumpa Samuel Umtiti ofa ya mkataba mpya kumfanya kuzifikiria Manchester United na Manchester City. (Daily Mail)

Borussia Monchengladbach wametoa ofa ya pauni milioni 10 kwa ajili ya kumnasa beki wa klabu ya West Ham, Reece Oxford.

Stoke City wameagiza skauti wao kumfanyia uchunguzi mshambuliaji wa klabu ya Celtic, Moussa Dembele.

Wilfried Zaha anasema kwamba hatondoka Crystal Palace kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 120 kwa ajili ya kumnasa mchezaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard.

Watford wanafikiri kutoa pauni milioni 3 kwa ajili ya kumnasa golikipa wa klabu ya Getafe, Vicente Guaita.

Leon Goretzka
Juhudi za Arsenal na Liverpool kumsajili Leon Goretzka zimechochewa baada ya wakala wa kiungo huyo wa Schalke 04 kukanusha taarifa zilizodai nyota huyo yuko tayari kujiunga na Bayern Munich.

Beki wa klabu ya Wolves, Kortney Hause anawaniwa na klabu za Huddersfield na Watford. (Sun)

Liverpool itahitaji fedha nyingi zaidi kutoka Barcelona kabla ya kufikiria kumruhusu Philippe Coutinho aondoke Anfield. (Telegraph)

Golikipa wa Southampton, Alex McCarthy ametuma ujumbe kwa Fraser Forster kwamba hata ikatia tamaa nafasi yake kirahisi. (Express)

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekana kuwepo tofauti kati ya mshambuliaji wake, Alexis Sanchez na wachezaji wenzake. (Sky Sports)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 2 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 2 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/02/2018 06:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.