Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 1 Januari, 2018

Luis Suarez
Tottenham wanapanga kutumia fedha watakayoingiza baada ya kumuuza Harry Kane kufanikisha usajili wa mshambuliaji Luis Suarez kutoka Barcelona.

Real Madrid wako tayari kuuza wachezaji zaidi ya wawili akiwemo na Gareth Bale ili kuhakikisha uhamisho wa Neymar unafanikiwa. 

Wachezaji wenye majina makubwa katika klabu ya Real Madrid wamepinga mpango wa klabu hiyo kutaka kumsajili winga kutoka Valencia, Goncalo Guedes. (Don Balon)

Klabu ya Real Madrid inaandaa ofa ya pauni milioni 130 kwa ajili kumnasa nyota wa Chelsea, Eden Hazard.

West Ham wameambiwa watatakiwa kulipa kiasi cha pauni milioni 40 ili kumpata beki wa klabu ya Swansea, Alfie Mawson.

Paulo Dybala
Manchester United wana matumaini kwamba, kiungo wa klabu hiyo, Paul Pogba anaweza kufanikisha uhamisho wa mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala.

Rangers wana jaribu kumshawishi chipukizi wa klabu ya Arsenal, Marcus McGuane ajiunge nao kwa mkopo.

Klabu za Derby, Birmingham na Sunderland zimejiunga na klabu ya Cardiff kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya straika wa Norwich, Cameron Jerome.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anamtaka kiungo wa kati wa Inter Milan, Joao Mario aje kuziba pengo la Michael Carrick. (Sun)

Antoine Griezmann
Jose Mourinho anataka kumsajili Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid mwezi Januari, kuinusuru Manchester United katika msimu huu ambao una msikukosuko kwao, na ameiomba bodi ya klabu hiyo kuhakikisha uhamisho huo unafanikiwa. (Express)

Southampton wanakazania usajili wa Theo Walcott kutoka Arsenal kwa uhamisho wa mkopo.

Kuelekea kukamilika kwa dili lake la kujiunga na klabu ya Everton akitokea Besiktas, mshambuliaji wa Uturuki, Cenk Tosun ameonekana London siku ya mwaka mpya.

West Brom wameulizia uwepo wa uwezekano wa uhamisho wa golikipa wa  Manchester United, Sam Johnstone, huku Crystal Palace na West Ham pia zikionyesha nia ya kutaka saini yaek. (Daily Mail)

Nottingham Forest wanatazamia kumteua Aitor Karanka achukuwe nafasi ya Mark Warburton, ambaye alifukuzwa siku ya mwisho wa mwaka 2017. (Times)

West Brom wanaandaa ofa kwa ajili ya beki wa kati wa klabu ya Middlesbrough,  Ben Gibson, ambaye anaweza kuwa chaguo lao la kwanza kwa ajili kuziba pengo la Jonny Evans.

Watford wana uhakika wa kushinda vita ya kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Leicester, Islam Slimani.

Theo Walcot
Arsenal wanaweza kumuchia Theo Walcot aondokae, huku Everton, Watford na West Ham zikionyesha nia ya kumsajili nyota huyo.

Adrian yuko tayari kujitoa na kusaini mkataba mpya katika klabu ya West Ham sasa baada ya kurejea kwenye nafasi yake ambayo ilikuwa imechukuliwa na Joe Hart.

Burton Albion wana nia ya kumsajili chipukizi wa klabu ya Crystal Palace, Jordon Mutch. (Mirror)

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekana kuwepo kwa tofauti kati ya mshambuliaji wa timu hiyo, Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 29 na wachezaji wenzake. (Sky Sports)

Celtic wako tayari kuto ofa kwa ajili ya usajili wa beki wa Dundee, Jack Hendry.

Burnley wanaweza kujaribu kumsajili beki wa Celtic, Jozo Simunovic mwezi Januari. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 1 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 1 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/01/2018 04:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.