Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 8 Januari, 2018

Antoine Griezmann
Antoine Griezmann atahitaji kulipwa mshahara wa pauni milioni 400,000 kwa wiki ili kuikatisha tamaa Barcelona na badala yake aende Manchester United.

Meneja wa Cardiff, Neil Warnock ana tazamia uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Bournemouth, Lewis Grabban.

Fulham inatarajiwa kumsajili beki wa Southampton, Matt Targett kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Real Madrid wako tayari kuwafanya nyota wawili wa Chelsea, Eden Hazard na Thibaut Courtois kuwa vinara kwenye orodha yao ya wachezaji inaowahitaji kwenye majira ya joto.

Manchester United wamepewa uhuru wa kusajili Alex Sandro baada ya Chelsea kuijiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota huyo wa Juventus.

Jese Rodriguez ana karibia kukamilisha taratibu za uhamisho kwenda katika klabu yake ya nyumbani, Las Palmas kumaliza wakati wake mgumu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Thorgan Hazard
Klabu ya Chelsea iko tayari kuongeza Hazard mwingine kwenye kikosi chao kwa kumrejesha mdogo wake na Eden, anayeitwa Thorgan.(Sun)

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema kwamba, klabu yake haitakuwa na uwezo wa kumlazimisha mshambuliaji wake, Harry Kane abaki.

Conte: Barkley anatakiwa akazanie nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza. (ESPN)

Liverpool watafuatilia uwezekano wa kumrejesha Naby Keita kutoka RB Leipzig. Klabu hiyo ilipia pauni milioni 5 kwa ajili ya uhamisho wa kiungo huyo kwenye majira ya joto na kumwacha abakie kwa mkopo katika klabu ya Leipzig kama sehemu ya mipango yao.

Jake Clarke-Salter
Beki wa klabu ya Chelsea, Jake Clarke-Salter anatarajiwa kukamilisha taratibu za uhamisho kwenda Sunderland. Nyota huyo aliichezea Uingereza kwenye kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 20 na alikaribia kujiunga na klabu ya Birmingham kwa mkopo kwenye majira ya joto.

Southampton watajaribu kufanya makubaliano na klabu ya Arsenal kuhusiana na uhamisho wa Theo Walcott kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Chelsea imemhakikishia Ruben Loftus-Cheek kuwa bado ana nafasi, licha ya kwamba klabu hiyo imemsajili Ross Barkley kutoka Everton kwa pauni milioni 15.

Graham Potter
Kocha wa Ostersunds, Graham Potter ameibuka na kuwa kinara kwenye orodha ya makocha wanaotarajiwa kupewa kazi ya umeneja katika klabu ya Stoke City.

Rafa Benitez hana mategemeo mengine zaidi ya kufanikiwa kusajili wachezaji wa mkopo pekee, ikiwa mazungumzo ya kuinunua klabu ya newcastle kati ya Mike Ashley na Amanda Staveley yanaendelea kuwa magumu. (Daily Mail)

Liverpool haitapoteza muda kujaribu kumasjili Riyad Mahrez au Thomas Lemar mwezi Januari, licha ya kumuuza Philippe Coutinho kwenda Barcelona.

Mauricio Pochettino anakiri kwamba, uhamisho wa Philippe Coutinho kutoka Liverpool kwenda Barcelona unaonyesha ni jinsi gani ilivyo ngumu kwa klabu kuwabakisha wachezaji wao wenye kiwango cha juu, lakini anasisitiza kwamba Harry Kane anaweza kumuiga shujaa wa Roma, Francesco Totti kwa kubakia Tottenham hadi mwisho wa maisha yake ya soka.

Wesley Sneijder 
Wesley Sneijder amekamilisha taraitibu za uhamisho kwenda Al-Gharafa ya Qatar kwa mkataba wa miezi 18.

Golikipa wa Stoke City, Jack Butland ameitaka klabu yake ifanye usajili wa wachezaji wapya kwenye dirisha la usajili mwezi Januari. (Sky Sports)

Manchester United wameanzisha mazungumzo juu ya uhamisho wa beki wa klabu ya Chelsea, David Luiz mwezi huu.

Arsene Wenger amejiandaa kumruhusu straika wa Arsenal, Alexis Sanchez kwenda Manchester City mwezi Januari, ikiwa klabu hiyo itafanikiwa kumnasa winga wa  Leicester, Riyad Mahrez achukuwe nafasi yake. (Mirror)

Crystal Palace wanakazania uhamisho wa golikipa wa Getafe, Vicente Guaita, lakini wanakumbana na ushindani mkubwa kutoka Watford.

Jonny Evans
Arsenal inakaribia kumsajili beki na nahodha wawa klabu ya West Brom, Jonny Evans. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 8 Januari, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 8 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/08/2018 10:58:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.