Loading...

Rais Magufuli ainyoshea kidole Wizara ya Madini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewabadilikia baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano na kuwataka kutenda kazi kama atakavyo yeye kwani wasipofanya hivyo maana yake nafasi hizo haziwafai tena.

Magufuli amesema hayo leo wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kudai kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki pamoja na Naibu wake Stanslaus Nyongo na kuwataka kubadilika mara moja.

"Bado Wizara ya Madini haifanya kazi vizuri sana najua nikizungumza kwa kupamba nitakuwa mnafiki Mhe. Spika utatambua mwezi wa 7 Bunge lilipitisha sheria ya madini kubadilisha ile sheria iliyokuwepo mkapitisha sheria namba 7 ya mwaka 2017 ambayo Bunge na Watanzania wengi tuliamini kwamba kupitia sheria hii mambo mengi ya nchi yangenyooka ikiwa pamoja na kupata mlahaba na kupata faida na madini yetu. Ile sheria ilipofika nilisaini na kuwapa maelekezo watendaji wangu kuandaa 'regulations' lakini mpaka sasa ni miezi saba imepita regulations hazijasainiwa" alisema Rais.

Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa kutokana na vitendo hivyo vya wateule wake ni wazi kuwa kuna matatizo makubwa ndani ya Serikali.

"Unaweza kujiuliza kuwa tuna matatizo makubwa ndani ya Serikali, kwa sababu kama regulations zile hazijasaini mnategemea nini? Kuanzia mwezi wa saba hawakusaini leo tupo mwezi wa kwanza bado hazijasainiwa, usipokuwa na regulations mtu yoyote atakapo default atapelekwa kwenye mahakama gani? Kwa hiyo sisi Watanzania baadhi ya watendaji wa Serikali hawapo makini ninasema hii kwa uchungu mkubwa baadhi ya niliowateua bado hawajanielewa ninataka nini" alisisitiza Rais.

Pia Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ambaye sasa yupo likizo "unapokuja kukumbushwa kwamba kuna haya mabaya kwenye eneo lako na wewe upo maana yake ni kwamba hufiti, unatakiwa wewe uyagundue kabla ya watu wengine kuyagundua kwa hiyo Wizara ya Nishati mnachangamoto kubwa bado mengi hayajafanyika. Wizara ya Madini mkajirekebishe mfanye kazi kiukweli mpaka sasa Wizara ya Madini haija ni 'impress' na mumfikishie salamu hizi waziri bado haja ni 'impress' lakini nategemea mtabadilika" alisisitiza Rais.
Rais Magufuli ainyoshea kidole Wizara ya Madini Rais Magufuli ainyoshea kidole Wizara ya Madini Reviewed by Zero Degree on 1/08/2018 02:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.