Loading...

Video: Mabingwa watetezi wa FA Cup, Arsenal walivyochapwa goli 4-2 na Nottingham Forest


Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Arsenal imeondolewa katika michuano hiyo kwa kichapo cha goli 4-0 dhidi ya Nottingham Forest inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.

Magoli mawili kutoka kwa beki wa Nottingham Forest, Eric Joseph Lichaj na magoli mengine mawili kutoka kwa Per Mertesacker na Dan Welback yalizifanya timu hizo hadi mapumziko kuwa sare ya goli 2-2.

Makosa waliyoyafanya mabeki wa Arsenal yakazalisha penati mbili zilizopingwa na Ben Brereton na Kieran Dowell zikawamaliza Arsenal na kuwaondosha kwenye mashindano hayo kwa goli 4-2. 


Matokeo mengine ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo:

  • Newport 2-1 Leeds
  • Shrewsbury 0-0 West Ham
  • Tottenham 3-0 AFC Wimbledon 
Video: Mabingwa watetezi wa FA Cup, Arsenal walivyochapwa goli 4-2 na Nottingham Forest Video: Mabingwa watetezi wa FA Cup, Arsenal walivyochapwa goli 4-2 na Nottingham Forest Reviewed by Zero Degree on 1/08/2018 03:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.