Loading...

TFF yafanya mabadiliko ya muda wa mechi ya Azam FC na Yanga SC


Mechi kati ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC imerudishwa masaa nyuma na hatimaye kuchezwa saa 10 Alasiri badala ya muda ule wa awali saa 1:00 usiku kama ilivyokuwa.

Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kupitia Afisa Habari wake, Cliford Mario Ndimbo na kusema mchezo huo utachezwa saa 10 siku ya Jumamosi (Januari 27, 2018) katika viwanja vya Azam Complex Chamanzi vilivyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Aidha, Afisa huyo alisema viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni shilingi elfu kumi (10,000) kwa jukwaa kuu na shilingi elfu saba (7,000) kwa majukwaa ya kawaida.

Kwa upande mwingine mchezo huo utarajiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka Dar es Salaam ambapo muamuzi wa kati ni Israel Nkongo akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na mwamuzi msaidizi namba mbili Soud Lila, mwamuzi wa akiba Elly Sasii wakati Kamishna wa mchezo huo ni Omar Abdulkadir.
TFF yafanya mabadiliko ya muda wa mechi ya Azam FC na Yanga SC TFF yafanya mabadiliko ya muda wa mechi ya Azam FC na Yanga SC Reviewed by Zero Degree on 1/24/2018 11:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.