Loading...

CCM yaibuka kidedea Ubunge Kinondoni na Siha

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia
TUME ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Maulid Mtulia wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Ubunge, Jimbo la Kinondoni baada ya kupata kura 30,313 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Salum Mwalim (CHADEMA) aliyepata kura 12,353 na Rajab Salum wa CUF aliyepata kura 1,943.

“Kwa matokeo hayo na kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na sheria ya uchaguzi, namtangaza Maulid Mtulia kuwa Mbunge wa Kinondoni,” amesema msimamizi huyo wa uchaguzi.

Jana jioni Februari 17,2018 Kagurumjuli alisema kazi ya kutangaza matokeo ingekamilika saa sita usiku lakini hilo lilishindikana.

Ulinzi uliimarishwa katika eneo la kujumlisha matokeo la Biafra, ambako Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa; Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi wamekesha katika eneo la kuhesabu kura.

Mgombea wa CCM, Maulid Mtulia naye alikesha eneo hilo akisema hataki kuuchukulia kirahisi uchaguzi huo.


Wawakilishi wa vyama vya upinzani hawakuwepo eneo hilo.

Mgombea Dkt. Godwin Mollel (CCM) ameibuka mshindi wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro uliofanyika jana Jumamosi, Feb 17, 2017.

Ikitangaza matokeo hayo, Tume ya Uchaguzi (Nec), imesema Dkt. Mollel amepata kura 25,611 dhidi ya kura 5,905 alizopata Elvis Mosi wa CHADEMA, kura 274 alizopata Tumsifueli Mwanri wa CUF na kura 170 alizopata Azaria wa SAU.

Matokeo ya Uchaguzi Kinondoni
CCM yaibuka kidedea Ubunge Kinondoni na Siha CCM yaibuka kidedea Ubunge Kinondoni na Siha Reviewed by Zero Degree on 2/18/2018 04:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.