Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 18 Februari, 2018
Keylor Navas |
Keylor Navas anatambua kwamba ni vigumu kuhamia katika klabu ya Real Madrid baada ya klabu hiyo kuonyesha mapenzi yao kwa Cortouis na David de Gea, na kwa sasa matumaini yake ni ya kujiunga na Chelsea au Manchester United. (Don Balon)
Klabu ya Chelsea inaweza kumwacha Michy Batshuayi aondoke moja kwa moja kwenda Borussia Dortmund kama watampata nyota wa timu ya taifa ya Marekani, Christian Pulisic. (ESPN)
Meneja wa klabu ya Barcelona, Victor Valverde amefurahishwa na kitendo cha timu yake kuwa makini na kuifunga Eibar, kuliko kukosa umakini kwa kuiwaza mechi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea wiki ijayo.
Francis Coquelin ameifungia Valencia goli lake la kwanza tangu kujiunga na klabu hiyo ya Uhispania mwezi Januari.
Cesc Fabregas amewataka wachezaji wenzake wa Chelsea wasimdharau kiungo wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta kwa kigezo cha umri wake katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa. (Sky Sports)
Sadio Mane |
Meneja wa Brentford, Dean Smith ataanza kufanya mazungumzo na klabu hiyo juu ya mkataba mpya wiki ijayo.
Golikipa wa Fluminense, Diego Cavalieri anatarajia kusani mkataba wa miaka mitatu katika klabu ya Crystal Palace wiki hii.
Manchester City inatazamia kumsajili kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund, Julian Weigl.
Shujaa wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta amesema Luis Enrique atang'ara kama atachukua madaraka ya kuinoa Chelsea. (Mirror)
Nyota wa klabu ya Tottenham wanahofu kuwa Toby Alderweireld anaondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Timo Werner amekiri kuwa angependelea kuichezea Manchester United au Manchester City.
Paulo Dybala |
Nyota wa klabu ya Juventus, Paulo Dybala amerejea mazoezini kuelekea mechi yao ya pili ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Tottenham.
Meneja wa klabu ya Tottenham, Moaurcio Pochettino ana mpango wa kuwasajili nyota wawili wa klabu ya Watford, Richarlison na Abdoulaye Doucoure kwa kiasi cha pauni milioni 50.
Manchester City inatrajiwa kumpa ofa ya mkataba mpya beki wake chipukizi, Oleksandr Zinchenko.
Golikipa wa klabu ya Burnley, Nick Pope ndiye chaguo la kwanza la Newcastle United kwa sasa.
Klabu ya West Ham inakaribia kumnasa kiungo wa klabu ya Saint-Etienne, Jonathan Bamba.
Tottenham na Arsenal zinashindania saini ya chipukizi wa klabu ya Stevenage, Ben Wilmot. (Sun)
Kiungo wa Tottenham, Victor Wanyama ana matumaini ya kutimiza ndoto za ke za utotoni katika soka kwa kushinda taji la FA. (Telegraph)
Mtoto wa mmiliki wa Arsenal, Josh Karaoke atafanya ukaguzi katika klabu hiyo kufanya maandalizi ya maisha ya baadae baada ya Arsene Wenger.
Jose Mourinho anasema kuwa hajui kama Paul Pogba atakuwa fiti kuivaa Sevilla kwenye Ligi ya Mabingwa.
Cesc Fabregas na Lionel Messi wakiwa pamoja na wake zao |
Cesc Fabregas anakiri kuwa Lionel Messi amekuwa kimya sana kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 18 Februari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
2/18/2018 12:09:00 PM
Rating: