Loading...

Klabu ya Ligi Kuu ya Ufaransa yatangaza kumsajili mtoto wa Didier Drogba


Klabu ya soka ya En Avant de Guingamp ambayo inashiriki ligi kuu ya Ufaransa, imetangaza kumsajili mchezaji Isaac Drogba (17) amabye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba.

Isaac amewahi kucheza katika chuo cha soka cha Chelsea nchini Uingereza.

Kupitia mtandao wa Instagram, Drogba ameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo kubwa aliyopiga mwanae kwa kuandika, “Kwako wewe najivunia zaidi @isaacdrogba11 @eaguingamp Fiers de toi @isaacdrogba11 @eaguingamp.”

Frank Lampard ambaye amewahi kucheza na Drogba katika timu ya Chelsea, kupitia mtandao huo ame-comment kwa kuandika, “Hongera! Namkumbuka Isaac kama kijana mdogo mtaratibu! Sasa amekuwa mwanaume!.”

Naye John Terry hakutaka hilo limpite akaamua kuandika, “Siwezi kuamini kama amekuwa kiasi hicho, hongera.”
Klabu ya Ligi Kuu ya Ufaransa yatangaza kumsajili mtoto wa Didier Drogba Klabu ya Ligi Kuu ya Ufaransa yatangaza kumsajili mtoto wa Didier Drogba Reviewed by Zero Degree on 2/20/2018 09:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.