Loading...

Mnyama amemaliza kazi nchini Djibouti


Klabu ya Simba wakiwa ugenini nchini Djibouti wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendarmerie, bao la Simba likiwekwa langoni na mshambuliaji wa Kimataifa Raia wa Uganda, Emmanuel Okwi dakika ya 53 ya mchezo huo.

Mechi hiyo imekuwa na ushindani mkubwa na Simba wamepoteza nafasi za tatu za kufunga za wazi huku wenyeji Gendamerie wakipoteza moja.

Simba wameonekana kushambulia lakini Gendamerie wako makini nao wamekuwa wakijibu mashambulizi tofauti na mechi ya kwanza ambayo walifungwa kwa mabao 4-0 mjini Dar es Salaam.
Mnyama amemaliza kazi nchini Djibouti Mnyama amemaliza kazi nchini Djibouti Reviewed by Zero Degree on 2/20/2018 08:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.