Loading...

Mamlaka ya Hali ya Hewa [TMA] yatao tahadhari


Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa hali mbaya ya hewa katika maeneo yote ya pwani kuanzia leo usiku mpaka Februari 7 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumatatu) na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa taarifa kamili angalia hapo chini:

Mamlaka ya Hali ya Hewa [TMA] yatao tahadhari Mamlaka ya Hali ya Hewa [TMA] yatao tahadhari Reviewed by Zero Degree on 2/05/2018 05:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.