Loading...

Liverpool inamtaka nyota huyu wa Arsenal kwenye majira ya joto


Liverpool iko tayari kujaribu kumshawishi Jack Wilshere atue Anfield kwa kumpa ofa ya mkataba wenye maslahi zaidi ya mkataba wake wa sasa katika klabu ya Arsenal.


Klabu hiyo inaripotiwa kuwa na matamanio mkubwa ya kumsajili Jack Wilshere kama kiungo huyo atagoma kusaini mkataba mpya Arsenal. Washika bunduki hao wamempa Wilshere mkataba mpya lakini wanataka kupunguza mshahara wake kutokana na historia yake ya majeruhi.

Jack Wilshere
Mkataba wa kiungo huyo wa Timu ya Taifa ya Uingereza katika klabu ya Arsenal unaisha mwisho wa msimu huu na hivi sasa yuko kwenye mazungumzo na klabu hiyo juu ya mkataba mpya.

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp yuko tayari kumnasa nyota huyo na amejianda kumlipa mshahara sawa na anaolipwa kwa sasa, ikiwa ni juhudi za kumfanya ahamie Anfield.

Inasemekana Klopp anamtamani sana kiungo huyo na anamchukulia kama mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Emre Can. Hivi karibuni meneja huyo wa Liverpool alikiri kwamba, hana uhakika kama Can atasaini mkataba mpya.

Kama Jack Wilshere atakubali uhamisho huo, atafuata nyayo za Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Arsenal kwenye majira ya joto.
Liverpool inamtaka nyota huyu wa Arsenal kwenye majira ya joto Liverpool inamtaka nyota huyu wa Arsenal kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 2/05/2018 05:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.